Friday 1 May 2015

DC HAI “ACHENI KUINGIZA SIASA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO”.


kaika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Ndg Antony Mtaka akizungumza katika uchaguzi wa wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe
picha na Edwine Lamtey 0758129821




myenyekiti mpya wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe Michael Sitaki Mmasi


mhandisi wa maji wilaya ya Hai Eng. Nyakaraita Mwita akizungumza na wajumbe wa mkutano wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe.

Grace Makiluli katibu tawala msaidizi serikali za mitaa mkoani Kilimanjaro.

HAI
MKUU wa wilaya ya Hai Antony Mtaka amempongeza aliyekuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Mstaafu Erasto N kweka  kwa jitihada zake alizozifanya wakati akihudumu kama askofu ikiwamo kupokea miradi mbli mbali ya maji iliyopitia katika Dayosisi Hiyo.
Mtaka ameyasema hayo hii leo wakati wa kikao cha  kumchagua mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe kilichofanyika katika shule ya sekondari Lyamungo.
Amesema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuiletea jamii maendeleo pasipokuwa na ukiritimba, ubadhirifu na kuweka maslai binafsi ya shughuli za kimaendeleo.
“ ni jambo la bahati sana kwa Askofu Kweka kutanguliza maslai ya Wananchi katika mradi huu wa maji pasipo kujali atanufaika vipi, ingekuwa ni mtu asiyekuwa mwadilifu angegeuza mradi kuwa wake huku wananchi wakiangamia kwa ukosefu wa maji safi na salama.” Alisema Mtaka
“Askofu Kweka alipoke Euro mill. 34 sawa na shilingi Bill. 68 mwaka 1992 ambapo ndipo mradi huo ulianza rasmi ukijumuisha vijiji 11 kutoka Hai na Vijiji 13 kutoka Moshi vijijini, ingekuwa ni mwingine angepeleka wapi?”  Alihoji Mtaka
Sanjari na hayo amewataka viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza bodi hiyo ya Lyamungo Umbwe kuepuka kuchanganya siasa na kazi za miradi ya maendeleo ili miradi hiyo iweze kuwanufaisha wananchi wote na vizazi vya baadae.
“epukeni kutapeliwa na wanasiasa wanaojiingiza katika miradi ya kimaendeleo kwani wengi wao ni wapotoshaji kwa kuingiza siasa katika utendaji” alisema Mtaka.
Kwa upande wake mhandisi wa maji wilaya ya Hai ambaye pia alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo Mhandisi Nyakaraita Mwita amewataka wajumbe waliochaguliwa katika bodi hiyo kupeanan ushirikianano katika utendaji ikiwemo pamoja na kushirikiana na halmashauri ili  kuleta ufanisi zaidi.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuopata maji safi na salama kama bodi ya maji ilivyojusudia ili kuepuka mnagonjwa mbali mbali yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.
Pia amesema kuwa wanawake wamekuwa ni waathirika wakubwa wa utafutaji wa maji safi na salama katika familia zao jambo linalowapelekea kushindwa kushiriki katika  shughuli nyingine za kimaendeleo.
Katika zoezi la upigaji wa kura wajumbe walikuwa 258 ambapo kura moja iliharibika huku Michael Sitaki Mmasy akishikilia nafasi ya mwenyekiti,Emmanuel Izack Show akiwa ni makamu mwenyekiti ambapo walipita bila kupingwa kutokana na kutojitokeza kwa wagombea wengine kuchukua fomu za nafasi hizo kama ilivyotakiwa.
Kwa upande wa wajumbe watendaji wa bodi ya maji, Bibianna Mmasy aliibuka mshindi kwa kupata kura 85 na Bi, Joyce Kweka akipata kura 71 ambazo zote kwa pamoja zilivuka asilimia hamsini iliyoitajika.

Habari na Edwine Lamtey $ Davis Minja

MADIWANI HAI WACHACHAMAA, WADAI KUMBUKUMBU SAHIHI ZA ARDHI.




Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Hai limewataka wataalamu wa ardi kutoka nje ya kikao cha baraza hilo na kuleta taarifa sahihi zinazohusiana na ni hekari ngapi ambazo zinamilikiwa na halmashauri katika eneo la mashine Tools na ni majina ya wamiliki yafahamike.
Katika kumbukumbu amabazo zilizowasilishwa katika kikao cha baraza hilo zinaonyesha kuwa halmashauri hiyo inamiliki hekari 17 jambo ambalo lilitolewa maelekezo katika baraza lililopita na kusemekana ni hekari 27 ikiwa na maana kwamba taarifa ilikosewa kuandikwa.
Kati kikao cha leo kwenye kumbukumbu imeonyesha tena ni hekari 17 badala ya 22 ambapo Mh. Rajabu Nkya diwani wa kata ya Machame Mashari amehoji kuwa`` kuna aina fulani ya udanganyifu unaoendelea katika mashamba ya Mashine Tools tunamwomba afisa ardhi atuletee taarisa sahihi kabla ya kumalizika kwa kikao hichi na ikiwa inaonyesha majina ya wamiliki” ``kamati iundwe ili kubaini ukweli na uhalali wa mashamba hayo kwa wamiliki”
Baada ya mvutana wa muda mrefu iliundwa kamati ya watu sita watatu wakiwa ni waheshimiwa madiwani na watatu kutoka katika upande wa wataalam na kupewa wiki mbili katika kushughulikia jambo hilo.
katikati ya watatu waliovaa miwani ni Mbunge Viti maalum Jimbo la Hai Mh. Grace kiwelu akisoma kabrasha la kikao cha madiwani.
picha na Edwine Lamtey 0758-129821
 


mbunge wa Viti maalumu jimbo la Hai Mh. Lucy Owenya akichangia mjadala kuhusiana na hoja ya mapato ya halmashauri 60% kutengwa kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo ambapo awali madiwani walitaka kujua ni sababu gani zinakwamisha miradi mingine ya maendeleo katika wilaya kutoendelea hadi sasa
picha na Edwine Lamtey 0758-129821
  
katikati ya picha ni mwenyekiti wa baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Hai ndg. Clement   Kwayu, kulia ni makamu mwenyekiti Ally Mwanga na kushoto kwake ni mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Melkizedeck Humbe
picha na Edwine lamtey 0758-129821
  
Kushoto katika meza kuu ni Mkuu wa wilaya ya Hai Ndg. Antony Mtaka akizungumza katika kikao cha  baraza la madiwani  ikiwa ni mara yake ya kwanza mara baada ya kupata uhamisho toka Mvomero Morogoro kuja Wilaya ya Hai

picha na Edwine lamtey 0758-129821









Thursday 12 March 2015

BREAKING NEWS:


 Ajali imetokea changalawe Mafinga basi la Majinja lilikuwa linatokea Mbeya kwenda Dar limeangukiwa na kontena muda huu na watu wengi wanakadiriwa kufariki na hali ni mbaya sana
Watu wapatao 50 wanahofiwa kufa papo hapo baada ya basi hilo la Majinja Express kugongana na lori na kuangukiwa na kontena

Friday 6 March 2015

BRN MAFANIKIO ZAIDI









Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela akiwa katika picha ya pamoja kati ya waalimu na  wakufunzi  katika semina ya ufunguzi wa matokeo makubwa sasa (BRN)  wilayani Same

Picha Na,
James Gasind 



Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh Ane Kilango Malecela amewataka waalimu wa shule za msingi waliyo pewa mafunzo ya mbinu bora ya ufundishaji kutumia elimu hiyo ili kunyanyua elimu hapa nchini.

Aliyasema hayo wiki hii wilayani Same alipokuwa katika ufunguzi wa mpango  wa uboreshaji  wa utekelezaji wa matokeo makubwa sasa BRN  ambapo umekutanisha  Wilaya Tano ambazo hazikuweza kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2012.

Malechela alizitaja halmashauri zilizo husika kupokea mafunzo hayo bora ya ufundishaji ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Rombo,Same,Moshi vijijini,Handeni na Korogwe.

Aliongeza kuwa elimu na mafunzo waliyo pata itasaidia kuboresha elimu katika shule za msingi kwani uwepo wa vitendea kazi pamoja na majengo kuwapo pasipo kuwa na waalimu wanao pewa mafunzo mara kwa mara hakutaweza saidia kuinua elimu hapa nchini ndio maana utekelezaji wa matokeo makubwa sasa umeanza kwa kuwapa waalimu mafunzo na mbinu mpya za ufundishaji.

“Ndugu Waalimu tukisema kuwa tulete vitabu pamoja na miundo mbinu mizuri kuwekwa shuleni pasipo Waalimu kupewa mafunzo mara kwa mara ya mbinu na namna ya ufundishaji ili kukuza taaluma na kuongeza ufauli wa Wanafunzi hapa Nchini bado tutakuwa hatuja piga hatua katika sekta ya Elimu”Alise Malechela.

Alisema kuwa takribaniWilaya 40 zitapokea mafunzo hayo lengo likiwa ni kuwapa waalimu wa masomo ya Hisabati,Kiswahili na Kiingereza mbinu mbadala za kufundisha wanafunzi na kuwagundua mapema wanafunzi ambao wanahitaji msaada zaidi katika kupewa elimu ili kuwe na uwiano mzuri darasani.

Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo Lawrence Mwinuka aliipongeza serikali katika kutekeleza sera ya Matokeo makubwa sasa ambapo amewataka waalimu waliyo pokea mafunzo hayo kufanyia kazi pamoja na kuwafundisha waalimu wengine hatimaye kujenga kizazi chenye matumaini katika elimu ya uhakika.

“Tunashukuru kwa kukumbukwa hasa waalimu hawa wa masomo ya Hesabu,Kiingereza na Kiswahili ambapo ni masomo ambayo kwa namana nyingine yanawapa shida Wanafunzi wa shule za Msingi kilichopo ni sisi Waalimu kufanyia kazi mafunzo haya ili kuleta ushindani  wa ufaulu kwa Shule zetu”Alisema Mwinuka.

Naye Mkuu wa kitengo cha habari toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Sylivia Lupembe alisema kuwa mpango  uliopo ni kuhakikisha elimu hapa nchini inathaminiwa na kukua kwa kasi ili kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali.

Ilikuhakikisha sera ya matokeo makubwa sasa  BRN inafanikiwa kama ilivyo kusudiwa kwa kiwango kikubwa Malaka ya Elimu Tanzania imetoa wakufunzi 18 toka wizara ya elimu watakao zunguka nchi nzima kutoa elimu kwa halmashauri 40 ambazo hazikufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba 2012 ambapo kiasi cha shilingi milioni 137 zitatumika katika kutoa elimu kwa mafunzo hayo.

Habari Na 
Davis Minja 0769-432367


MCHEZAJI APOTEALEASHIMONI, MASHABIKI WAMSAKA






mchezaji wa Timu ya KIA FC akitoka katika shimo alilodumbukia  wakati akicheza mechi ambayo timu ya Kia Fc ilitinga hatua ya Fainali baada ya kuiadhibu timu ya Oasis mabao 3-1 mchezo ambao pia ulighubikwa na vurugu zilizosababisha refarii wa mchezo huo pamoja na mwamuzimsaidi wakijikuta wanaangukia kipigo.




baadhi ya mashabiki wa timu za Kia Fc na Oasis ambazozinashiriki michuano ya Fuya Cup wilayani Hai wakishuhudia tukio la mchezaji kutumbukia katika moja kati ya shimo lililopo katika uwanja wa CCM bomang'ombe







mashabiki wakielekea katika eneo la tukio ambapo mchezaji alitumbukia kwenye shimo lenye ukubwa wa zaidi ya mita 8

Picha na
Edwine Lamtey 0758-129821

AISHI KWA KUFUNGWA MIGOMBANI MIAKA SABA





bibi anayetuhumiwa  kumfunga mjukuu wake mgombani katika shina la kahawa huko katika kijiji cha Tela kata ya Machame Narumu wilayani  Hai Mkoani Kilimanjaro aelezea kisa hicho. 

picha na Edwine Lamtey.

MTOTO wa Kike anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka kumi na tano na kumi na sita(15-16)katika Kitongoji cha Ngundeni  Kijiji cha Tela Kata ya Machame Narumu Wilayani Hai Mkoani Kilimanjarao ameishi kwa kufungwa na kamba migombani kwa miaka saba huku akila chakula na Mbwa,Paka na Kuku wanao pita eneo hilo.

Tukio hilo la aina yake limewashituwa wakazi wa kijiji hicho Wilayani Hai kutokana na mtoto huyo kutoweka ghafla kwa kufichwa na Bibi wa upande wa Baba na baadae kuonekana tena katika hali iliyo jaa ukatili wa kutisha .

Akizungumza na BOMA HAI FM Mwenyekiti wa Dawati la Watoto na Jinsia Wilaya ya Hai Happy Eliufoo alisema kuwa Mtoto huyo aligundulika kutokana na msamaria mwema aliye muona mtoto huyo kafungwa katika shina la mgomba  na kamba miguuni huku akila chakula katika mazingira yasiyo ridhisha hivyo kuamua kutoa taarifa kwa kituo hicho.

Alisema kuwa kwa taarifa za awali Mtoto huyo ambaye ni yatima anayeishi na Bibi yake huyo alikuwa akisoma na wenzake ambapo alifika darasa la tatu kisha kutoweka ghafla ambapo baada ya kupatikana katika hali hiyo walio kuwa wanafunzi wenzake wali pigwa na butwaa.

Mtoto huyo huyo hutolewa asubuhi na kufungwa mgombani ambapo bibi yake huendelea na  shughuli zake za kila siku huku jua na mvua zikimuishia akiambulia kula chakula kilicho wekwa katika ndoo iliyo katwa na inapo timia majira ya usiku mara baada ya Bibi yake kurudi katika kazi zake hutolewa na kufungwa ndani karibu na Ng’ombe na Mbuzi.

Eliufoo aliongeza kuwa kitendo cha mtoto huyo kufichwa shambani huko kumempelekea mtoto huyo kuathirika Kisaikolojia kwani mpaka kwa sasa hapendi kuangalia watu usoni na hata kuongea inampa shida.
Akielezea hali ya kuishi kwa mtoto huyo Bibi yake aliye jitambulisha kwa jina la Anthonia Ngowi alisema kuwa aliamua kuishi na mjukuu wake huyo baada ya Baba yake  na Mama yake  kufariki mwaka 2009.

“Mtoto huyu ni mkorofi sana kwa hali hiyo huni lazimu kumfunga na kamba kwani hujisaidia kisha kupaka haja kubwa ndani”alisema Bibi yake.

Alipo hojiwa na zaidi juu ya kumfunga Mtoto huyo karibu na mifugo hiyo huku akijua wazi kuwa ni kosa kumfanyia Mtoto vitendo vya ukatili Bibi huyo alidai kuwa huwa anafanya hivyo ili kuzuia mifugo yake kuibiwa na wezi hivyo mtoto huyo kutumika kama Mlinzi.

Awali akitoa ufafanuzi wa Ukatili huo Bibi huyo alidai kuwa Mtoto huyo kabla ya kufiwa na Baba yake aliugua ugonjwa wa degedege hivyo kupelekwa kwa Mganga wa jadi ambapo Bibi huyo alisema kuwa alipona ila Mganga huyo hakumaliziwa pesa yake elfu thelethini ndipo ugonjwa huo ulipo mrudia tena.

“Kweli nasema ukweli kuwa ndiyo sababu ya Mtoto huyu kuwa hivi mimi siyo mshirikina na wala siyo mchawi nimemfungia mtoto huyu miaka saba shambani kwani sikupata msaada toka kwa ndugu zangu hata kwa watoto wangu”alidai Bibi huyo jambo ambalo lilizidi kuwachanganya watu.

Kwa upande wake Mwenyekiti na Mwanaharakati washirika lisilokuwa lakiserikali linalo jihusisha na utetezi wa wanawake na watoto Messe Ndossi alisema kuwa jambo hilo kwa Wilaya ya Hai ni lakusikitisha licha ya elimu kutolewa kila siku juu ya haki ya Mtoto na Malezi yaliyo bora.

“kwa kweli bado tunahitaji kutoa elimu hasa vijijini kufichua unyama na ukatili unao tendeka kwa watu wasio kuwa na sauti kama hawa ili kuweza kujenga kizazi ambacho siyo tegemezi siku za baadae,hivyo kila mmoja aweze kutimiza wajibu wake kwa kupinga ukatili”alisema Ndossi.

Aliongeza kuwa jamii inatakiwa kutojihusisha na imani za kishirikina kwani kwa kufanya hivyo wanajikuta wakifanya ukatili kwa watu wasiyo kuwa na hatia,huku akihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Mtoto huyo alichukuliwa nakupelekwa hosipitali ambapo alibainika kuwa na ugonjwa wa( UTI) kisha kupatiwa matibabu na kupelekwa katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa uangalizi wa karibu  huku Bibi yake akishikiliwa kwa mahojiano zaidi juu ya tuhuma za kumfanyia Mtoto ukatili huo.

Uelewa wa masuala ya ulinzi kwa mtoto Wilaya ya Hai utafiti ulibani kuwa ni 85%,pamoja na uelewa wa jamii kuwa juu kiasi hicho lakini bado kuna tatizo kubwa la ukiukwaji wa haki za watoto halii inamaanisha kuwa ama jamii inapuuzia jambo hili au tabia na mitazamo haijabadilika licha ya kuelewa.


Tafsiri yake ni kwamba,juhudi zinahitajika kuweka mikakati ya makusudi kuanzia ngazi ya familia,Kitongoji,Kijiji,Kata,Wilaya hadi Taifa kuhusu ukatili dhidi ya watoto.

APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA


MKAZI wa Tarakea Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro Joseph Minja (29) amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Hai kwa tuhuma za kukutwa  na madawa ya kulevya aina ya bangi yenye thamani ya shilingi milioni 155.

Akisoma hati ya Mashtaka mahakani hapo, Mwendesha mashtaka wa polisi Roymax Membe amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi katika eneo la Olmoloq Wilayani Siha akiwa anasafirisha kwenda nchi jirani ya Kenya.

Amesema mtuhumiwa alikamatwa na polisi mnamo Machi 3 mwaka  huu  majira ya saa 3 usiku  akiwa na bangi kiasi cha magunia kumi yenye jumla ya kilo 310 yenye thamani ya shilingi milioni   155

Amesema mtuhumiwa huyo ambaye pia ni dereva wa gari lililokutwa na bangi hiyo aina ya noah yenye namba za usajili T 470 BRC  inayofanya safari zake kutoka Moshi Mjini kuelekea Tarakea.

Hata hivyo, Membe ameieleza mahakama kuwa upelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika   na kumwomba hakimu kutoruhusu dhamana kutokana na kosa alilotenda mtuhumiwa  kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10


Kutokana na ombi hilo la mwendesha mashitaka, Hakimu Agnes Mhina aliharisha kesi hiyo hadi Machi 19 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa amepelekwa gerezani mpaka hapo kesi itakapotajwa tena.

NA
Mwandishi wetu