Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela akiwa katika picha ya pamoja kati ya waalimu na wakufunzi katika semina ya ufunguzi wa matokeo makubwa sasa (BRN) wilayani Same
Picha Na,
James Gasind
Naibu Waziri wa Elimu na
mafunzo ya ufundi Mh Ane Kilango Malecela amewataka waalimu wa shule za msingi
waliyo pewa mafunzo ya mbinu bora ya ufundishaji kutumia elimu hiyo ili
kunyanyua elimu hapa nchini.
Aliyasema hayo wiki hii wilayani Same alipokuwa katika
ufunguzi wa mpango wa uboreshaji wa utekelezaji wa matokeo makubwa
sasa BRN ambapo umekutanisha Wilaya Tano ambazo hazikuweza kufanya
vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2012.
Malechela alizitaja halmashauri zilizo husika kupokea
mafunzo hayo bora ya ufundishaji ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni
Rombo,Same,Moshi vijijini,Handeni na Korogwe.
Aliongeza kuwa elimu na mafunzo waliyo pata itasaidia
kuboresha elimu katika shule za msingi kwani uwepo wa vitendea kazi pamoja na
majengo kuwapo pasipo kuwa na waalimu wanao pewa mafunzo mara kwa mara
hakutaweza saidia kuinua elimu hapa nchini ndio maana utekelezaji wa matokeo
makubwa sasa umeanza kwa kuwapa waalimu mafunzo na mbinu mpya za ufundishaji.
“Ndugu Waalimu tukisema kuwa tulete vitabu pamoja na miundo
mbinu mizuri kuwekwa shuleni pasipo Waalimu kupewa mafunzo mara kwa mara ya
mbinu na namna ya ufundishaji ili kukuza taaluma na kuongeza ufauli wa
Wanafunzi hapa Nchini bado tutakuwa hatuja piga hatua katika sekta ya
Elimu”Alise Malechela.
Alisema kuwa takribaniWilaya 40 zitapokea mafunzo hayo
lengo likiwa ni kuwapa waalimu wa masomo ya Hisabati,Kiswahili na Kiingereza
mbinu mbadala za kufundisha wanafunzi na kuwagundua mapema wanafunzi ambao
wanahitaji msaada zaidi katika kupewa elimu ili kuwe na uwiano mzuri darasani.
Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo Lawrence Mwinuka
aliipongeza serikali katika kutekeleza sera ya Matokeo makubwa sasa ambapo
amewataka waalimu waliyo pokea mafunzo hayo kufanyia kazi pamoja na
kuwafundisha waalimu wengine hatimaye kujenga kizazi chenye matumaini katika
elimu ya uhakika.
“Tunashukuru kwa kukumbukwa hasa waalimu hawa wa masomo ya
Hesabu,Kiingereza na Kiswahili ambapo ni masomo ambayo kwa namana nyingine
yanawapa shida Wanafunzi wa shule za Msingi kilichopo ni sisi Waalimu kufanyia
kazi mafunzo haya ili kuleta ushindani wa ufaulu kwa Shule zetu”Alisema
Mwinuka.
Naye Mkuu wa kitengo cha habari toka Mamlaka ya Elimu
Tanzania Sylivia Lupembe alisema kuwa mpango uliopo ni kuhakikisha elimu
hapa nchini inathaminiwa na kukua kwa kasi ili kuzalisha wataalamu wa fani
mbalimbali.
Ilikuhakikisha sera ya matokeo makubwa sasa BRN
inafanikiwa kama ilivyo kusudiwa kwa kiwango kikubwa Malaka ya Elimu Tanzania
imetoa wakufunzi 18 toka wizara ya elimu watakao zunguka nchi nzima kutoa elimu
kwa halmashauri 40 ambazo hazikufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba
2012 ambapo kiasi cha shilingi milioni 137 zitatumika katika kutoa elimu kwa
mafunzo hayo.
Habari Na
Davis Minja 0769-432367
No comments:
Post a Comment