Grace Makiluli katibu tawala msaidizi serikali za mitaa mkoani Kilimanjaro.
HAI
MKUU wa wilaya ya Hai Antony Mtaka amempongeza aliyekuwa
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Mstaafu Erasto N kweka kwa jitihada zake alizozifanya wakati
akihudumu kama askofu ikiwamo kupokea miradi
mbli mbali ya maji iliyopitia katika Dayosisi Hiyo.
Mtaka ameyasema hayo hii leo wakati wa kikao cha kumchagua mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya
maji ya Lyamungo Umbwe kilichofanyika katika shule ya sekondari Lyamungo.
Amesema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kiongozi aliyekuwa
mstari wa mbele katika kuiletea jamii maendeleo pasipokuwa na ukiritimba,
ubadhirifu na kuweka maslai binafsi ya shughuli za kimaendeleo.
“ ni jambo la bahati sana kwa Askofu Kweka kutanguliza
maslai ya Wananchi katika mradi huu wa maji pasipo kujali atanufaika vipi,
ingekuwa ni mtu asiyekuwa mwadilifu angegeuza mradi kuwa wake huku wananchi
wakiangamia kwa ukosefu wa maji safi na salama.” Alisema Mtaka
“Askofu Kweka alipoke Euro mill. 34 sawa na shilingi Bill.
68 mwaka 1992 ambapo ndipo mradi huo ulianza rasmi ukijumuisha vijiji 11 kutoka
Hai na Vijiji 13 kutoka Moshi vijijini, ingekuwa ni mwingine angepeleka
wapi?” Alihoji Mtaka
Sanjari na hayo amewataka viongozi wapya waliochaguliwa
kuiongoza bodi hiyo ya Lyamungo Umbwe kuepuka kuchanganya siasa na kazi za
miradi ya maendeleo ili miradi hiyo iweze kuwanufaisha wananchi wote na vizazi
vya baadae.
“epukeni kutapeliwa na wanasiasa wanaojiingiza katika miradi
ya kimaendeleo kwani wengi wao ni wapotoshaji kwa kuingiza siasa katika
utendaji” alisema Mtaka.
Kwa upande wake mhandisi wa maji wilaya ya Hai ambaye pia
alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo Mhandisi Nyakaraita Mwita amewataka wajumbe
waliochaguliwa katika bodi hiyo kupeanan ushirikianano katika utendaji ikiwemo
pamoja na kushirikiana na halmashauri ili
kuleta ufanisi zaidi.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuopata maji safi
na salama kama bodi ya maji ilivyojusudia ili kuepuka mnagonjwa mbali mbali
yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi
na salama.
Pia amesema kuwa wanawake wamekuwa ni waathirika wakubwa wa
utafutaji wa maji safi
na salama katika familia zao jambo linalowapelekea kushindwa kushiriki
katika shughuli nyingine za kimaendeleo.
Katika zoezi la upigaji wa kura wajumbe walikuwa 258 ambapo
kura moja iliharibika huku Michael Sitaki Mmasy akishikilia nafasi ya
mwenyekiti,Emmanuel Izack Show akiwa ni makamu mwenyekiti ambapo walipita bila
kupingwa kutokana na kutojitokeza kwa wagombea wengine kuchukua fomu za nafasi
hizo kama ilivyotakiwa.
Kwa upande wa wajumbe watendaji wa bodi ya maji, Bibianna
Mmasy aliibuka mshindi kwa kupata kura 85 na Bi, Joyce Kweka akipata kura 71
ambazo zote kwa pamoja zilivuka asilimia hamsini iliyoitajika.
Habari na Edwine Lamtey $ Davis Minja
|
No comments:
Post a Comment