Wananchi mkoani Kilimanjaro wamekuwa na
taharuki ya ugonjwa wa ebola mkoani hapo baada aliyedaiwa kuwa mgonjwa wa ebola
kufikishwa katika kituo cha shirimatunda ambacho kimetengwa na mkoa kwa ajili
ya kushughulikia suala hilo .
Na kwa taarifa zilizopo hadi sasa ni mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amethibitisha kuwa “ni kweli kituo cha shirimatunda kimetengwa kwaajili ya watu
wenye ugonjwa wa ebola kufanyiwa uchunguzi, ila kwa mgonjwa aliyefikishwa hapo
amepimwa na kuonekana hana maambukizi ya ugonjwa huo ila alihisiwa na madaktari”
“alisema
Gama”
Hata hivyo mkuu huyo wa mkuu wa mkoa atakutana
na waandishi wa habari hii leo majira ya saa nne na imani ni kwamba
atazungumzia suala hili.
Endelea
kusikiliza redio Boma Hai Fm na kutufuatilia katika mtandao wetu kwa taarifa
zaidi.
Na
Edwine Lamtey 0758-129 821