Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema kwamba matokeo ya awali
ya aina mbili za chanjo dhidi ya maradhi ya Ebola yanatarajiwa kutolewa
mwishoni mwa mwaka huu.
Shirika hilo
limesema majaribio ya kitabibu yanayoendelea au yanayopangwa kufanywa Ulaya,
Afrika na Marekani, yanatarajiwa kurudisha data ifikapo mwishoni mwa mwezi
Desemba.
Naibu mkurugenzi mkuu wa WHO anayehusika na mifumo ya afya na utafiti
Dr Marie Paule Kieny amesema kwa uhakika majaribio hayo yataanza mnamo wiki
mbili zijazo.
Afisa huyo amesema matokeo ya majaribio ya chanjo hoizo mbili
zinazotoa matumaini, Chimp adenovirus na Chanjo ya VSV, yatakuwa ni ya mwanzo
tu, na kwamba majaribio hayo yataendelea kwa kipindi cha kati ya miezi sita
hadi 12.
Ameongeza hata hivyo kuwa malengo yao kwa sasa ni kuweza kutambua usalama wa
chanjo hizo, na kiwango cha dawa inayohusika katika chanjo yenyewe ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu.
NA DW SWAHILI
No comments:
Post a Comment