Waziri wa Uingereza anayehusika na maendeleo ya kimataifa
Justine Greening yuko ziarani nchini Sierra Leone , mojawapo ya nchi
zilizoathiriwa vibaya na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Waziri huyo ameandamana
na wanajeshi wapatao 100, ambao ni sehemu ya ujumbe wa msaada kutoka Uingereza
kusaidia katika mapambano dhidi ya Ebola.
Akizungumza mjini Freetown waziri
Greening amesema athari mbaya zaidi ya Ebola kwa Sierra Leone ni kukwama kabisa kwa
mfumo wa afya nchini humo.
Amesema pia kuwa ilikuwa inasikitisha kwamba
wahudumu wa afya walioongoza mapambano dhidi ya maradhi hayo walikuwa
wamepoteza maisha yao .
Waziri huyo amesema kuwa msaada wa nchi yake utakuwa muhimu
katika kukarabati mfumo wa afya wa Sierra Leone , na kuwapa matibabu
wauguzi pamoja na watu wengine walioambukizwa Ebola.
Tangu kuanza kwa mlipuko huu mpya wa Ebola magharibi mwa Afrika,
tayari watu zaidi ya 4500 wamekwishakufa, wakiwemo wahudumu wa afya wasiopungua
200.
Vifo vingi vimetokea katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi, ambazo ni Guinea , Liberia
na Sierra Leone .
No comments:
Post a Comment