Mazungumzo yanatarajiwa leo kati ya maafisa wa serikali ya Hong Kong na viongozi wa wanafunzi, katika juhudi za
kumaliza maandamano ya kudai demokrasia zaidi ambayo yamekuwa yakiendelea kwa
wiki tatu.
Wanaharakati wanataka uhuru kamili katika kuwachagua viongozi wa
kisiwa hicho ambacho ni sehemu ya China .
Hata hivyo China
inashikilia kuwa na kauli ya mwisho juu ya wagombea wa uchaguzi huo ambao
utafanyika mwaka 2017.
Pande zote katika mzozo huo zimeng'ang'ania misimamo yao , katika mgogoro huo ambao ndio mkubwa zaidi tangu
Uingereza ilipoikabidhi Hong Kong kwa China mwaka 1997.
No comments:
Post a Comment