Tuesday, 21 October 2014

HUKUMU DHIDI YA PISTORIUS KUTANGAZWA LEO

Hatma ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius itajulikanao leo. 

Jaji katika kesi ya mauaji inayomkabili atatangaza hukumu yake saa chache zijazo, ambapo anaweza kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani, au kifungo cha nyumbani na faini.

Pistorius alipatikana na hatia ya kumuuwa bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwezi Februari mwaka jana.

 Upande wa muendesha mashtaka ametaka apewe kifungo cha miaka 10 jela, huku mawakili wake wakipendekeza kifungo cha miaka mitatu, ambacho sehemu moja itakuwa kifungo cha nyumbani, na nyingine kazi za kuunufaisha umma.

Kesi yake imesabaisha mgawanyiko na hisia kubwa, na ni miongoni mwa zilizofuatiliwa sana nchini Afrika Kusini.
 NA DW SWAHILI

No comments:

Post a Comment