Thursday, 23 October 2014

WANANCHI WAMETAKIWA KUTOA TAARIFA ZA RUSHWA




WANANCHI wilayani siha mkoani kilimanjaro wametakiwa kutoa taarifa za rushwa katika maeneo yao ilikuhakikisha tatizo hilo linakwisha katika wilaya hiyo na taifa kwa ujumla

Wito huo imetolewa hivi karibuni na Mriamu Mayaya mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rusha Wilayani Siha  (TAKUKURU)wakati wa kikao cha DCC ,kilichfanyika katika ukumbi wa Rc Sanya juu

Mayaya alisema fushwa ni kikwazo katika kuendesha shudhuli za kimaendeleo kwa mujibu wa kifungu cha 16(1) ni kosa kwa mtu yoyote kutoa manufaa kwa ofisa wa umma kama ushawishi auzawadiilikupatiwamkataba

Pia ni kosa kwa mtu mwenye mamlaka kudai au kuomba fushwa ya ngono au upendeleo mwingine kwa mtu yoyote kama sharti la kutoa ajira ,kupandishwa cheo,kumpatia haki yake au huduma  maalum ni kwa mujibu wa kifungu cha 25  cha sheria

Alifafanua kuwa rushwa imejaa katika taasisi nyingi zikiwamo za serikali pamoja na za watu binafsi ,rushwa inaathiri kubwa kiuchumi kisiasa na kijamii,athari zitokanazo na vitendo vya rusha ni ukosefu wa huduma ya jamii kuongezeka kwa maovu katika jamii,ukosefu imani kwa serikali,uduma duni,uchaguzi wa viongozi wasiofaa,pato la taifa kupungua,kuongezeke kwa umasikini miongoni mwa jamii pamoja na kuongezeka kwa maambukiziyaukimwi

Wananchi mtuunge mkono katika suala hili bila kusita kwani rushwa ipomiongoni mwetu na maendeleo hayawezi kuja kama rushwa haitatokomezwa katika maeneo yetu pia taifa litayumba kimaendeleo

Alitoa wito kwa wananchi kuendeleo kutoa ushikianao pamoja na kutokua na hofu katika mapambano dhidi ya rushwa



No comments:

Post a Comment