Thursday, 23 October 2014

FANYIENI KAZI CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA


WANANCHI wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufanya uchambuzi wa changamoto za mazingira zilizopo ili waweze kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha mazingira ya wilaya hiyo yanatunzwa na kuwa katika hali nzuri muda wote.

Hayo yalisemwa na Maggece Simbaye ambaye ni Meneja wa the Dare Women's Foundation[DWF]kutoka mkoani Arusha wakati alipotombelea Taasisi ya TAKIMA inayojishughulisha na utetezi wa haki za jamii iliyopo katika Kijiji cha Nkusinde kata ya machame mashariki wilayani Hai amabapo pia walitundika mizinga 10 katika mto weru weru na kutembelea watoto yatima wa maeneo hayo.

Simbaye alisema suala la utunzaji mazingira siyo la mtu mmoja au kikundi flani,bali ni jukumu la watu wote ambalo linahitaji ushirikiano na uwajibikaji wa pamoja na wadau wote wanaohusika na uhifadhi wa mazingira.

Alisema ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,wananchi wanatakiwa kuepuka  ukataji miti hovyo,uchomaji moto wa misitu na uoto wa asili, kupanda miti na kuitunzapamoja na  kuthibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za viwandani na makazi

Kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya Takima andrea Njau amesema licha ya taasisi yake kujishughulisha na shughuli ya kutetea jamii pia wanajishughulisha na utunzaji  wa mazingira na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira

Sambamba na hilo wameanza mradi wa ufugaji wa nyuki katika kijijiji cha nkusinde katika mto weru weru na wameanza na mizinga kumi na matarajio ilikufikisha mizinga 300 ili kujiongezea ajira kwani ufugaji nyuki nimradi raisi  usio hitaji gharama kubwa na soko la asali linapatikana hivyo kuwataka wananchi kujiunga na mradi huo

NA MWANDISHI  WETU

No comments:

Post a Comment