Tuesday, 18 November 2014

CRDB- SIHA YAMWAGA MAGODORO,VYANDARUA NA SABUNI HOSPITALI YA KIBONG'OTO.




Benki ya CRDB inayomjali na kumsikiliza mteja kupitia tawi la Siha lililopo  mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Siha imewatembelea wateja wake katika hospitali ya Kibong’oto ambapo wamegawa magodoro,mashuka na sabuni kwa ajili ya watoto na kuahidi kuwa bado itaendelea kutoa misaada mbalimbali ili kujenga mahusiano makubwa zaidi na wateja wao.


Akikabidhi msaada huo mkurugenzi wa benki ya CRDB mkoa Kilimanjaro Fransis Moleli amesema kuwa banki hiyo inatambua umuhimu wa wateja wake hivyo kwa kupitia siku ya wateja duniani(CUSTOMER SERVICE WEEK) imeamua kutoa msaada huo ili kusema Asante kwa wateja wake.



Akipokea msaada huo daktari mkuu katika hospitali ya kibong’oto Dr. Kisonga Riziki amesema kuwa anaishukuru benki ya CRDB kwa msaada walioutoa hii ikiwa ni njia pekee ya kuendelea kuwajali wateja wake pamoja na kushiriki huduma za kijamii na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake meneja wa CRDB-Siha bi. Lightness Tarimo amesema kuwa katika kupanua huduma za kifedha CRDB ina mfumo wa kufanya miamala mbali mbali kwa njia ya simu iitwayo SIMBANKING hivyo ni vyema wananchi wakatumia fursa hiyo ili kujipatia huduma kwa urahisi. 

Pia amewakaribisha wafanyakazi wa hospitali hiyo  kujipatia  huduma mbalimbali kama vile mikopo,kufungua akaunti n.k
Aidha pia Bi. Lightness amesema kuwa msaada ambao umetolewa ni ishara ya kuonyesha kuwa  benki itazidi kushirikiana na hospitali hiyo pamoja na vyombo vingine vinavyotoa huduma kwa jamii ili kuimarisha mahusiano mazuri zaidi kwenye utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Hospitali ya kibong’oto ni hospitali maalumu ya kutoa huduma kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kifua kikuu na magonjwa mengine.
Na Edwine Lamtey

No comments:

Post a Comment