WITO
umetolewa kwa serikali kuepusha migogoro ya kimaslahi baina ya waalimu na
serikali kuwapa waalimu haki yao ya msingi ya kupata
mshahara kwa wakati.
Hayo
yamesemwa na katibu wa chama cha waalimu wilaya ya hai Samweli
Nyakrere wakati akizungumza na redio Boma Hai Fm ofisini kwake.
Amesema kuwa
kutokana na madai ya muda mrefu kutokea mwaka 2008 kutokupewa kipaumbele katika
kulipwa kwa wakati hali inayochangia kuwepo kwa migogoro baina ya serikali na
waalimu.
Ameongeza
kuwa katika upandishwaji wa madaraja kwa
waalimu bado hawapandishwi madaraja jambo linalo pelekea waalimu kukata tamaa
na kazi yao
huku sera ya serikali ikiwa ni matokeo makubwa sasa.
Kwa upande
wake meneja wa saccos ya waalimu wilaya ya hai bi. Pendo Lyatuma amesema kuwa kutokana na changamoto
mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa serikali wameweza kutoa mikopo kwa
riba nafuu kwa wafanyakazi wa serikali na wasio wa serikalini pamoja na kuwapa
mikopo waalimu kusoma na kuongeza elimu yao.
Aidha
Lyatuma ametoa wito kwa wanachama kuona umuhimu wa kuweka akiba katika saccos
wanazo kopa kwaajili ya kuwasaidia kwa maisha ya baadae.
Na Latifa Boto.
No comments:
Post a Comment