Mbunge Wa Jimbo
la Hai Mkoani Kilimanjaro Freeman Mbowe
amesikitishwa na kitendo cha mji mdogo wa hai kuendelea kuwa na uchafu, pamoja
na kwamba aliaznisha mpango wa kusafisha mji huo.
Akizungumza
na wananchi katika mkutano wa hadhara ulio fanyika katika mji mdogo wa bomang'ombe amesema kuwa kitendo
cha madiwani kushindwa kutekeleza
mpango wa kufanya usafi kimemsikitisha jambo ambalo limemlazimu kutafuta
mbinu mbadala.
Mbowe
amesema pamoja na viongozi hao kushindwa
kusimamia suala hilo
la usafi ameamua kuweka mikakati thabiti itakayo saidia kuondokana na hali ya
mji kuwa mchafu kwa kutoa vitendea kazi mbalimbali kwaajili ya kufanyai usafi.
Amefafanua
kuwa ili kukabiliana na hali ya uchafu
ametoa gari la kubeba taka lenye tani 30 kwaajili ya kubeba taka katika masoko
mbalimbali ndani ya wilaya ili kunusuru afya za walaji na wafanya biashara
wanaotoa huduma mbalimbali katika masoko yaliyo ndani ya wilaya ya hai kama vile soko la walaji Hai mjini, soko la masama mula, soko la kalali pamoja na masoko mengine.
Akizungumzia
suala zima la huduma ya afya amesema kuwa ili kuondokana na tatitio la gari
maalumu la kubebea wagonjwa (ambulance) ameahidi kutoa gari la wagonjwa kwa hosipitali
teule ya Machame na katika hosipitali ya wilaya ya Hai.
Mh. Mbowe ameongeza
kuwa katika kuhakikisha kuwa njia zina fanyiwa ukarabati wa kiwango kinacho
ridhisha na kufungua njia nyingine kwaajili ya manufaa ya wananchi ametoa
greda itakayo baki ndani ya wilaya siku zote kwa kuchimba na kuchonga
barabara ndani ya wilaya nzima ya Hai ili kurahisisha usafiri.
Aidha pia Mbowe
amewataka wananchi kuchagua viongozi waadilifu na watenda haki katika
uchaguzi wa mwezi ujao desemba wa
uchaguzi wa viongozi wa serikali ya mitaa ili waeweze kutetea haki ya
mtanzania.
Na Devis Minja.
picha na Edwine Lamtey.
No comments:
Post a Comment