Afisa biashara wa Halmashauri ya wilaya ya Hai bwana Halfan Kimaro akizungumza na wananchi waliohudhuria katika ufunguzi wa ofisi za mobisol wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kulia kwake ni Mwendesha tawi la mobisoli Tawi la Bomang’ombe Abubakari Mohamed
hizi ni baadhi ya bidhaa za Mobisol ikiwemo solar tv ya mobisol na vifaa vingene kwaajili ya nishati hiyo
picha na Edwine Lamtey
MOBISOL YAANGAZA WILAYA YA HAI
WANANCHI wilayania Hai Mkoani Kilimanjaro wameshauriwa kuepuka usumbufu wa upatikanaji wa nishati uliopo kwa kutumia sola ili kurahisisha gharama na kuepuka usumbufu.
Rai hiyo imetolewa leo na Afisa Biashara wa wilaya ya Hai Kimaro alipokuwa akizindua ofisi ya kampuni ya sola ya Mobisol ili kurahisisha na kuwapatia wananchi wa mjini na vijijini huduma ya umeme wa sola.
Kimaro amesema kuwa tatizo la Umeme limekuwa likiwakosesha wananchi kufanya mambo yao muhimu hasa yakimaendeleo yanayo hitaji nishati huku hali ya idadi ya Wakazi wilayani Hai ikiongezeka siku hadi siku.
Amesema kuwa ni vema kila Mwananchi kulinda kipato chake na kuondokana na tatizo la umeme katika maeneo yao kwa kuwa na huduma ya sola hiyo huku wakiambatanisha na nishati nyingine kama tahadhari na kwa matumizi mengine.
Awali Mwendesha tawi la mobisoli Tawi la Bomang’ombe Abubakari Mohamed amewataka wananchi wa Hai na viunga vyake kutumia pesa kwa malengo huku wakipata huduma ya nishati ya Sola kwa bei nafuu ili kulinda kipato cha Familia
Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kukumbuka pia wazazi wao walio vijijini kwa kuwapatia nishati ya Umeme wa Sola ili waweze kufanya mambo yao wawapo vijijini kwani upatikanaji wa umeme baadhi ya vijijini umekuwa ni shida.
Habari na Davis Minja 0769432367
WATU wa wili wakazi wa wilaya ya Hai Kijiji cha Uduru Machame Mkoani Kilimanjaro wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi.
Akisoma hukumu hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai Denis Mpelembwa,Mwendesha Mashtaka wa Polisi Inspekta Simon Feo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hendry Loti Masawe mwenye umri wa miaka 30 na mwenzake Abiudi Jubilet Shilewangwa mwenye umri wa miaka 35 wote wakazi wa Machame.
Aidha watuhumiwa hao wamekutwa na hatia hiyo baada ya ushahidi uliokuwa kukamilika ambapo watuhumiwa hao walitenda kosa hilo huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria ambapo pia mshitakiwa wa kwanza Hendry Loti Massawe ni shemeji wa Mwanafunzi huyo.
Kesi hiyo kwa mara ya kwanza iliripotiwa katika Dawati la Jinsia La Wilaya Ya Hai chini ya Mwenyekiti wa dawati hilo Happyness Eliufoo ambapo ilifikishwa mahakamani kwa upelelezi zaidi hadi upelelezi ulipo kamilika na kutolewa kwa hukumu.
Awali watuhumiwa hao walimbaka Mwanafunzi huyo kwa zamu Disemba 26 mwaka 2013 huko katika kijiji cha Uduru Machame Wilayani Hai ambapo shemeji yake Hendry Loti Massawe alimshawishi kutoka naye wakasherehekee sikukuu ambapo ilikuwa kinyume kisha kumbaka nakumsababishia maumivu makali.
Mwenyekiti wa dawati la polisi wilaya ya Hai Happyness Eliufoo amesema kuwa ni vyema taarifa zaidi zikaendelea kutolewa kwa wale wanaofanya ukatili na unyama dhidi ya binadamu na kusema kuwa huku hii pia ni fundisho kwa wale wenye tabia kama hizi.
Habari na Devis Minja 0769-432367
No comments:
Post a Comment