bibi anayetuhumiwa kumfunga mjukuu wake mgombani katika shina la kahawa huko katika kijiji cha Tela kata ya Machame Narumu wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro aelezea kisa hicho.
picha na Edwine Lamtey.
MTOTO wa
Kike anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka kumi na tano na kumi na sita(15-16)katika
Kitongoji cha Ngundeni Kijiji cha Tela
Kata ya Machame Narumu Wilayani Hai Mkoani Kilimanjarao ameishi kwa kufungwa na
kamba migombani kwa miaka saba huku akila chakula na Mbwa,Paka na Kuku wanao
pita eneo hilo.
Tukio hilo
la aina yake limewashituwa wakazi wa kijiji hicho Wilayani Hai kutokana na
mtoto huyo kutoweka ghafla kwa kufichwa na Bibi wa upande wa Baba na baadae
kuonekana tena katika hali iliyo jaa ukatili wa kutisha .
Akizungumza
na BOMA HAI FM Mwenyekiti wa Dawati la Watoto na Jinsia Wilaya ya Hai Happy
Eliufoo alisema kuwa Mtoto huyo aligundulika kutokana na msamaria mwema aliye
muona mtoto huyo kafungwa katika shina la mgomba na kamba miguuni huku akila chakula katika
mazingira yasiyo ridhisha hivyo kuamua kutoa taarifa kwa kituo hicho.
Alisema kuwa
kwa taarifa za awali Mtoto huyo ambaye ni yatima anayeishi na Bibi yake huyo
alikuwa akisoma na wenzake ambapo alifika darasa la tatu kisha kutoweka ghafla
ambapo baada ya kupatikana katika hali hiyo walio kuwa wanafunzi wenzake wali
pigwa na butwaa.
Mtoto huyo
huyo hutolewa asubuhi na kufungwa mgombani ambapo bibi yake huendelea na shughuli zake za kila siku huku jua na mvua
zikimuishia akiambulia kula chakula kilicho wekwa katika ndoo iliyo katwa na
inapo timia majira ya usiku mara baada ya Bibi yake kurudi katika kazi zake
hutolewa na kufungwa ndani karibu na Ng’ombe na Mbuzi.
Eliufoo
aliongeza kuwa kitendo cha mtoto huyo kufichwa shambani huko kumempelekea mtoto
huyo kuathirika Kisaikolojia kwani mpaka kwa sasa hapendi kuangalia watu usoni
na hata kuongea inampa shida.
Akielezea
hali ya kuishi kwa mtoto huyo Bibi yake aliye jitambulisha kwa jina la Anthonia
Ngowi alisema kuwa aliamua kuishi na mjukuu wake huyo baada ya Baba yake na Mama yake
kufariki mwaka 2009.
“Mtoto huyu
ni mkorofi sana kwa hali hiyo huni lazimu kumfunga na kamba kwani hujisaidia
kisha kupaka haja kubwa ndani”alisema Bibi yake.
Alipo hojiwa
na zaidi juu ya kumfunga Mtoto huyo karibu na mifugo hiyo huku akijua wazi kuwa
ni kosa kumfanyia Mtoto vitendo vya ukatili Bibi huyo alidai kuwa huwa anafanya
hivyo ili kuzuia mifugo yake kuibiwa na wezi hivyo mtoto huyo kutumika kama Mlinzi.
Awali akitoa
ufafanuzi wa Ukatili huo Bibi huyo alidai kuwa Mtoto huyo kabla ya kufiwa na
Baba yake aliugua ugonjwa wa degedege hivyo kupelekwa kwa Mganga wa jadi ambapo
Bibi huyo alisema kuwa alipona ila Mganga huyo hakumaliziwa pesa yake elfu
thelethini ndipo ugonjwa huo ulipo mrudia tena.
“Kweli nasema
ukweli kuwa ndiyo sababu ya Mtoto huyu kuwa hivi mimi siyo mshirikina na wala
siyo mchawi nimemfungia mtoto huyu miaka saba shambani kwani sikupata msaada
toka kwa ndugu zangu hata kwa watoto wangu”alidai Bibi huyo jambo ambalo
lilizidi kuwachanganya watu.
Kwa upande
wake Mwenyekiti na Mwanaharakati washirika lisilokuwa lakiserikali linalo
jihusisha na utetezi wa wanawake na watoto Messe Ndossi alisema kuwa jambo hilo
kwa Wilaya ya Hai ni lakusikitisha licha ya elimu kutolewa kila siku juu ya
haki ya Mtoto na Malezi yaliyo bora.
“kwa kweli
bado tunahitaji kutoa elimu hasa vijijini kufichua unyama na ukatili unao
tendeka kwa watu wasio kuwa na sauti kama hawa ili kuweza kujenga kizazi
ambacho siyo tegemezi siku za baadae,hivyo kila mmoja aweze kutimiza wajibu
wake kwa kupinga ukatili”alisema Ndossi.
Aliongeza
kuwa jamii inatakiwa kutojihusisha na imani za kishirikina kwani kwa kufanya
hivyo wanajikuta wakifanya ukatili kwa watu wasiyo kuwa na hatia,huku
akihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Mtoto huyo
alichukuliwa nakupelekwa hosipitali ambapo alibainika kuwa na ugonjwa wa( UTI)
kisha kupatiwa matibabu na kupelekwa katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi
katika mazingira magumu kwa uangalizi wa karibu
huku Bibi yake akishikiliwa kwa mahojiano zaidi juu ya tuhuma za
kumfanyia Mtoto ukatili huo.
Uelewa wa
masuala ya ulinzi kwa mtoto Wilaya ya Hai utafiti ulibani kuwa ni 85%,pamoja na
uelewa wa jamii kuwa juu kiasi hicho lakini bado kuna tatizo kubwa la ukiukwaji
wa haki za watoto halii inamaanisha kuwa ama jamii inapuuzia jambo hili au
tabia na mitazamo haijabadilika licha ya kuelewa.
Tafsiri yake
ni kwamba,juhudi zinahitajika kuweka mikakati ya makusudi kuanzia ngazi ya
familia,Kitongoji,Kijiji,Kata,Wilaya hadi Taifa kuhusu ukatili dhidi ya watoto.
No comments:
Post a Comment