MKAZI wa Tarakea Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro
Joseph Minja (29) amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Hai kwa tuhuma za
kukutwa na madawa ya kulevya aina ya
bangi yenye thamani ya shilingi milioni 155.
Akisoma hati ya Mashtaka mahakani hapo, Mwendesha
mashtaka wa polisi Roymax Membe amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na
polisi katika eneo la Olmoloq Wilayani Siha akiwa anasafirisha kwenda nchi
jirani ya Kenya.
Amesema mtuhumiwa alikamatwa na polisi mnamo Machi 3
mwaka huu majira ya saa 3 usiku akiwa na bangi kiasi cha magunia kumi yenye
jumla ya kilo 310 yenye thamani ya shilingi milioni 155
Amesema mtuhumiwa huyo ambaye pia ni dereva wa gari
lililokutwa na bangi hiyo aina ya noah yenye namba za usajili T 470 BRC inayofanya safari zake kutoka Moshi Mjini
kuelekea Tarakea.
Hata hivyo, Membe ameieleza mahakama kuwa upelezi wa
kesi hiyo bado haujakamilika na
kumwomba hakimu kutoruhusu dhamana kutokana na kosa alilotenda mtuhumiwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni
10
Kutokana na ombi hilo la mwendesha mashitaka, Hakimu Agnes
Mhina aliharisha kesi hiyo hadi Machi 19 mwaka huu itakapotajwa tena na
mtuhumiwa amepelekwa gerezani mpaka hapo kesi itakapotajwa tena.
NA
Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment