Wananchi wilayani hai mkoani Kilimanajaro wametakiwa
kuisoma na kuielewa katiba pendekezwa na hatimaye kuipigia kura ili kupata
katiba mpya yenye kukidhi matakwa ya wananchi.
Hayo yamesemwa hii leo na mkuu wa wilaya mshikizi
Novatus Makunga ambaye pia ni muu wa wilaya ya Moshi wakati wa uzinduzi wa
katiba pendekezwa uzinduzi ambao
umehudhuriwa na viongozi wa serikali na taasisi mbali mbali zisizo za
kiserikali.
Makunga amesema kuwa ni vyema wananchi wakatumia
muda wao kuzisoma nakala za katiba pendekezwa zitakazotolewa katika maeneo yao
na kuepukana na watu wanaoizungumzia katiba hiyo pendekezwa bila ya kuwa na uelewa wa kile
kilichoandikwa.
Awali akimkaribisha mkuu wa wilaya mshikizi,
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Melkizedeck Humbe amesema
kuwa nakala hizo zitagawiwa katika kata, vijiji, zahanati, hospitali, vyuo na
taasisi mbali mbali bila kusahau vijiwe mbali mbali vilivyopo wilayani hapa
huku pia akimtaka kila mwananchi kuisoma katiba hiyo pendekezwa.
Naye mwenyekiti wa baraza la madiwani wa Hai Clement
Kwayu amesema kuwa mwananchi ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ambapo maamuzi hayo
yatatolewa katika kura ya maoni ambapo kila mwananchi atapata fursa ya
kushiriki kuipigia kura.
Kwa upande wake afisa habari wa wilaya ya Hai bi.
Rizik Lesuya amesema kuwa wananchi watapata kuielewa katiba pendekezwa hasa
ukizingatia halmashauri ya Hai inamiliki kituo cha redio Boma hai Fm ambacho
kitafanya kazi ya kuuelimisha umma juu ya katiba pendekezwa kupitia vipindi
vyake.
NA
Edwine Lamtey 0758-129821
No comments:
Post a Comment