JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT ), Wilaya Siha mkoani Kilimanjaro umevunja chama cha Akiba na mikopo cha Jumuiya hiyo kutokana na viongozi wake kushindwa kukiendesha cha hicho.
Imeelezwa kuwa Saccos hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 ikiwa na wanachama 115 imevunjwa na Viongozi wa UWT Wilaya Siha kutokana na viongozi wa Saccos hiyo chini ya mwenyekiti wake, Denengwa Deole wameshindwa kuendeleza kwa takribani miaka 7
Akizungumza na mwandishi wa radio Boma Hai, katibu wa UWT wilayani Siha, Zeydani Mwamba amesema kuwa wameamua kuvunja saccos hiyo kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa wanachama wake ambapo wamesema kuwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho hakuna wanachama wapya wala mikopo iliyoweza kuchangishwa na viongozi hao
Mwamba amesema pamoja na chama hicho kuanzishwa kwa lengo la kuboresha hali ya wanachama ili kujikwamua kiuchumi kwa kupatiwa mikopo ya masharti nafuu ,wamefikia maamuzi hao ili kuondoa mgogoro ambao ungeweza kujitokeza kutoka na fedha za wanachama hao kukaa mda mrefu bila ya kufanyiwa kazi.
Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa kwa sasa wameanza kurejesha fedha za wanachama wote ambao walichangia tangu mwaka 2007 ili kuweza kuweka mfumo mzuri na mipango ya baadae kwa ajili ya kuanzisha kwa upya
NA Devis Minja.
No comments:
Post a Comment