JAMII imetakiwa kuhakikisha ina wajibu wa kulinda rasimali za umma na kupambana na kila aina ya uovu ukiwemo ubadhirifu wa wizi rushwa na mengineyo ili kuweza kunufaika nazo na kuwaletea maenendeleo yao.
Ushauri huo umetolewa na msimazi wa miradi Chama cha waalimu wa masomo ya Uraia Tanzania, (CETA) Goodluck Justine baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa kamati za ufuatiliaji wa rasimali za umma (PETS) ngazi za kijiji kurejeshwa fedha kiasi cha zaidi ya milioni 1.2 zilizokuwa zimechangwa na wananchi kujereshwa kwa ajili shughuli za kimaendeleo.
Justine alisema endapo jamii inajengewa mfumo mzuri wa kufuatlia miradi na kujua fedha zilizotolewa na Halmashauri zao katika utekelezaji miradi husika itasaidia kuwaezesha kutambua na kuelewa namna ya kukabiliana na viongozi ambao wameshindwa kusimamia utekeleza na kusababisha kutekelezwa kwa miradi chini ya kiwango.
Akizungumza na wajumbe wa kamati za PETS wakati wakipokea mrejesho wa kazi zilizofanywa na wajumbe hao wa ngazi za vijiji vilivyopatiwa mafunzo kwa wawezeshaji wa CETA Taifa yaliyofanyaika katika ukumbi wa halmshauri ya Wilaya ya Hai.
Wamesema mafanikio yaliyopatika mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo, mjumbe wa kati ya PETS kutoka kijiji cha Tella, Alloyce Kweka alisema kuwa wameweza kurejesha fedha kiasi cha shilingi 945,000 zilizokuwa zimechangwa kwa ajili mradi wa shule ya sekondari ya Tella pamoja na ujenzi wa choo cha shule iliyopo kijiji hapo.
Kweka alisema hizo zilichangwa na kukaa bila ya kutumia kwa mda mrefu na bila kutolewa maelezo hali ambayo ilisababisha kuleta maswali mengi kwa wananchi lakini PETS ilifuatilia na hatimaye kurejeshwa na kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Nae Mjumbe wa PETS kutoka kijiji cha Ussari alisema kamati hiyo ilifuatilia na kubaini kuwa jumla ya vocha za pembejeo zaidi 9 zenye thamani ya shilingi 352,000 zilizokuwa zimetolewa kinyume na taratibu zimeweza kujeshwa kwa kaya husika baada ya wajumbe wa kamati kuzitoa kaya ambayo si husika.
Nae Mratibu wa CETA, Safari Minja alisema wameamua kutoa mafunzo hayo ili wananchi wajitambue na kufahamu wajibu wao kufuatilia fedha na rasilimali za umma.
Hata hivyo walishauri ni vyema jamii ikapewa mafunzo ya kuwajengea ufahamu wa kuhoji mapato na matumizi, hasa idara zinazogusa moja kwa moja jamii; Elimu, maji, miundo mbinu na afya.
NA
Omary Mlekwa
No comments:
Post a Comment