Tuesday, 21 October 2014

WAJANE WATAKIWA KUTOKUWA TEGEMEZI.

Arusha

Wajane kote nchini wametakiwa kutokuwa tegemezi katika jamii pindi waume zao wanapofariki bali wajishughulishe na shughuli mbalimbali zitakazo waingizia kipato na kuweza kujikwamua kimaisha.

Wito huo umetolewa na Makamu wa Askofu Mkuu wa Makanisa ya Christian Life Tanzania {CLC} Askofu Joseph Laizer wakati wa kongamano la wanawake na wajane lililofanyika katika kanisa la Sinai Pentekoste Mlima wa Washindi Mkoani Arusha.

Askofu Laizer alisema kuwa wajane wakijishughulisha kwa shuguli mbalimbali wataweza kuendesha maisha yao ya kila siku na kuondokana na changamoto zinazowakabali ikiwamo unyanyasaji.

Kwa upande wake Salome Laizer mama mchungaji wa kanisa hilo wakati akifundisha neno la mungu alieleza kuwa ysu kristo ni msaada kwa wajane na nguzo yao hivyo wamtegemee katika kila jambo na yeye atawasaidia.

Alisema kuwa wajane hao wakiwa karibu na yesu kristo huku wakisimamia neno lake katika kudai haki zao wataweza kupata vyote wanavyovihitaji hivyo wasisite kumpelekea yesu shida zao kwani yeye atawasaidia.


NA mwandishi wetu.

No comments:

Post a Comment