Monday, 20 October 2014

MKURUGENZI AAGIZWA KUFUATILIA MIKATABA YA HALMASHAURI MOSHI.



BARAZA  la madiwani la halmashauri ya Manispaa ya Moshi,  mkoani Kilimanjaro, limemuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Shaaban Ntarambe, kufuatilia kwa karibu mikataba yote ambayo halmashauri hiyo inapoingia na wakandarasi.

Wakizungumza katika kikao maalumu cha baraza hilo, madiwani hao walisema mikataba mingi imekuwa ikisainiwa bila kufuata utaratibu jambo ambalo limesababisha miradi mingi kutokukamilika kwa wakati.

Diwani wa viti maalumu Mery Olomi, , alisema halmashauri hiyo iliingia mkataba na Hamieri T. LTD ya mjini Moshi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya karanga lakini hadi leo mkandrasi huyo hajakamilisha.

Diwani wa kata ya Ng’ambo Genesis Kiwelu alisema halmashauri nyingi zimekuwa zikipata hati chafu ambazo zinasababishwa na uingizaji wa mikataba hewa.

Kwa upande wake mkaguzi mkuu wa ndani mkoa wa Kilimanjaro, kutoka ofisi ya CAG, Joseph shirima, alisema wamebaini kuwepo kwa udhaifu katika halmashauri hiyo katika usimamizi wa mikataba.

Alisema udhaifu mkubwa walioubaini ni kuwa mikataba inayotolewa utekelezaji wake umekuwa hausimamiwi ipasavyo, na kongeza kuwa mratibu wa mradi ambaye anateuliwa na halmashauri hiyo, ni vyema akawa mwangalifu katika kuisimamia miradi hiyo.

Meya wa halmashauri hiyo Japhary Michael, aliwataka watendaji wa halmashauri,  kufuata taratibu za mikataba ili mambo hayo yasijirudie tena.

Naye Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Dkt Christopha Mtamakaya alisema ameipokea hoja hiyo na kwamba ataifanyia kazi katika vikao vijavyo vya baraza hilo na kuvitolea taarifa.
NA mwandishi wetu.

No comments:

Post a Comment