Monday, 20 October 2014

CAG MSTAAFU UTOUH WANANCHI JITOSENI KATIKA MAENDELEO MSIISUBIRIE SERIKALI PEKEE




ROMBO

MKAGUZI na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali, (CAG), mstaafu, Bw. Ludovick Utouh, ametoa rai kwa Watanzania hususan wadau wa elimu kuachana na dhana ya kuwa maendeleo yote yanatokana na serikali au michango ya wafadhili pekee.

Bw. Utouh alitoa rai hiyo juzi, alipotoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhi na uzinduzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Tarakea, iliyoko wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Bw. Utouh ambae alishirikiana na Bodi na uongozi wa shule hiyo kupata ufadhili huo, mbali na kuipongeza serikali ya Japan kwa msaada huo, pia aliwataka wanafunzi watakaonufaika na msaada huo kulipa fadhila kwa wafadhili hao kwa kufanya vyema katika mitihani yao mbalimbali.

Awali Mkuu wa shule hiyo Bw. Martin Kijja, alisema ujenzi wa bweni hilo umekuja wakati muafaka na kwamba utawanufaisha wanafunzi wa kike 64 ambao walikuwa wakitembea muda mrefu kwenda shuleni na hivyo kuwaepusha na adha mbalimbali ikwemo mimba wawapo mashuleni.

Kwa upande wake Balozi Mdogo wa Japan hapa nchini, Bw. Kazuyoshi Matsunaga, alisema Tanzania ina raslimali kuu mbili kwa sasa ambazo alisema ni pamoja na gesi ya asili na Wanafunzi wengi walioko mashueli.

NA mwandishi wetu.

No comments:

Post a Comment