Monday, 20 October 2014

BELLAVIEW NI LAZIMA MUWE WAZALENDO KUZALISH AJIRA ZAIDI



ROMBO

NAIBU Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Kazuyoshi Matsunaga,
amesema nchi yake inadhamini wawekezaji wazalendo ambao alisema kazi zao huongeza nafasi za ajira nchini.

Balozi Matsunaga aliyasema hivi karibuni katika wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, wakati alipokitembelea kiwanda cha kusindika matunda na uzalishaji maji cha Bellaview kilichopo wilayani humo.

Alisema kuwa nchi yake hudhamini wawekezaji wa namna hiyo na kwamba katika kudhibitisha hilo, huwa inatoa ushirikiano kupitia miradi
mbalimbali inayofanywa na shirika la kimataifa la ushirikiano nchini
humo, JICA.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho Bw. Shanel Ngowi, alisema kampuni hiyo ilianza uzalishaji miaka mitatu iliyopita pale kilipoanza kuzalisha maji ya kunywa.


Alisema kiwanda hicho kwa sasa kimetoa ajira za kudumu 150 wengi wao wakiwa ni wakazi wa wilaya ya Rombo na zingine zaidi ya 1,000 wakiwa ni vibarua wanaofanya kazi kiwandani hapo pamoja na wasambazaji wa bidha zinazozalishwa na kiwanda hicho walipo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumzia changamoto zinazokikabili kiwanda hicho, Bw. Ngowi
alisema ni pamoja upatikanaji wa malighafi chache haswa nyakati za
kiangazi jambo ambalo linasababisha hali ngumu katika kipindi hicho.
NA Edwine Lamtey


No comments:

Post a Comment