Serikali
wilayani Hai imewaasa wananchi kuachana na tabia ya unywaji wa pombe uliokithiri
ambao unaathiri nguvu kazi pamoja na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu
wa Wilaya ya Hai Novatus Makunga amesema kuwa wazazi pamoja na vijana wengi
wanaokaa vijiweni wakiowemo madereva wa “bodaboda” ndio kundi linalosadikiwa
kukithiri katika unywaji wa pombe aina ya gongo na viroba ambavyo vinatishia
kuathiri mfumo wa uzazi.
Amesema
kuwa pombe hizo ni kali, sio salama na hazina na nchi nzima inaweza kukosa
nguvu kazi kutokana na vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kupungua au
kutokuwa na nguvu ya kufanya kazi inavyopaswa kutokana na hali yao ya unywaji
wa pombe hizo zisizo salama.
Katika
kukabiliana na hali hiyo, Makunga amesema kuwa tayari wilaya yake ipo katika
hatua za mwisho kukamilisha sheria sheria ndogo ndogo inayopiga marufuku unywaji
wa pombe wakati wa saa za kazi wilayani humo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment