Monday, 20 October 2014

ASKOFU WA TAG TUSITEGEMEE WAFADHILI PEKEE


ASKOFU WA  TAG TUSITEGEMEE WAFADHILI PEKEE
 SIHA

WASHIRIKA katika makanisa mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuongoza katika harambee zinazofanywa kwenye makanisa yao na kuacha kutegemea wafadhili pekee kuwafanyia mambo kama hayo ya maendeleo.

Wito huo umetolewa na Askofu wa jimbo la Kilimanjaro wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG),Glorius Shoo wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya kanisa la TAG Sayuni lilipo wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ambapo pia kuliwa  na  harambe ya kuchangia ununuzi wa vyombo kwa ajili ya kuhubiria Injili wa kanisa wa kanisa hilo

Shoo alisema, uchangiaji kwenye shughuli za maendeleo usitegemee zaidi wafadhili, badala yake nguvu zaidi zitumike kwa wanaoandaa na wafadhili wasaidie kukamilisha shughuli iliyolengwa ambayo itakuwa na manufaa zaidi kwa wahusika.

Aidha, Askofu huyo  aliwaasa wananchi katika maeneo mbalimbali, kutumia rasilimali walizo nazo, kusaidiana katika kufanikisha suala la kuleta maendeleo kwenye maeneo husika badala ya kutegemea watu kutoka mbali kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo.

Hata hivyo katika maadhimisho hayo, pia kanisa hilo lilitoa vitu mbali mbali kwa ajili ya kusaidiwa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi  na yatima cha Matumaini kilichopo katika kijiji cha Koboko wilayani hapa.

NA Omary Mlekwa.


No comments:

Post a Comment