Serikali
wilayani siha mkoani kilimanjaro imewataka wananchi kuepuka ushawishi wa maneno
yanayotolewa kwa ajili ya kukwamisha zoezi la ujenzi wa maabara katika shule za
sekondari.
Kauli hiyo
imetolewa na mkuu wa wilaya ya siha ndugu Charles Mlingwa wakati akizindu
ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya fuka iliyopo kata ya Ivaen
wilayani Siha.
Amesema kuwa
kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishawishi wananchi kuto changia ujenzi kwa
madai kuwa suala hilo
ni jukumu la serikali jambo ambalo si kweli kwani kila mwananchi anajukumu la
kuchangia maendeleo kwenye eneo lake.
Amesema kuwa
kila mwananchi ana uwezo wa kuchangia zoezi hilo ili kuweza kukamilika kwa wakati.
Dr Mlingwa
amesema serikali haitawavumilia wale wote
ambao watakaobainika kukwamisha zoezi la ujenzi huo ambao unatarajiwa
kukamilika kabla ya November thelethini mwaka huu.
No comments:
Post a Comment