Zaidi ya
watoto mil.5wanatarajia kupata chanjo ya surua na rubell katika Halimashauri
saba za mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kutokomeza magonjwa ya ulemavu na vifo
vinavyosababishwa na magonjwa hayo.
Hayo
yamesemwa na Bw. Peter Kihamia mratibu wa chanjo katika Mkoa wa Kilimanjaro
wakatia akizungumza na waandishi wa habari katika kampeni shirikishi ya chanjo
ya surua na rubella ambayo inaendelea kitaifa .
Kihamia
amesema kuwa Chanjo hiyo itakuwa inawalenga watoto wenye umri wa miezi tisa
hadi miaka kumi na nne na miezi kumi na moja na itapunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa
yanayo sababisha ulemavu kwa watoto
pamoja na vifo vitokanavyo na magonjwa hayo.
Aidha
ameongeza kuwa kampeni hii ya kitaifa ya chanjo ya surua- rubella itawafikia
watoto wote ambao hawakupata chanjo kabla na wale ambao hawakupata kinga
kikamilifu ili kuzuia milipuko ya magonjwa hayo.
Naye Meneja mpango wa chanjo Taifa Bi. Dafrosa Lyimo
ameeleza kuwa mlundikano wa watoto wasio na kinga kila baada ya miaka mitatu
hadi minne huweza kusababisha mlipuko wa magonjwa.
Lyimo
amewashauri wazazi na walezi nchini kuondokana na imani potofu kuhusana swala
la chanjo kwani ni jambo la kitaifa na wazazi wahakikishe watoto wanapata fursa
iliyo jitokeza kwani kinga ni bora kuliko tiba.
NA LUCY ULOMI
No comments:
Post a Comment