Na katika michezo mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wameisambaratisha Roma ya Italia kwa
kuifunga magoli 7-1 katika mechi ya kundi E ya mabingwa wa Soka barani Ulaya,
Champions League.
Sherehe hiyo ya magoli ilianza katika dakika ya tisa ya mchezo
kwa bao la kusisimua lililoingizwa na mchezaji wa kiungo, Arjen Roben. Timu
nyingine ya Ujerumani iliyocheza jana, Schalke iliifunga kwa taabu Sporting
Lisbon iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani, kupitia mkwaju wa penalti uliotolewa
kwa njia yenye utata. Matokeo ya mwisho katika mechi hiyo ya kundi G yalikuwa
Schalke 4-Sporting Lisbon 3.
Kwingineko Chelsea ya Uingereza iliilaza Maribor magoli 6-0,
lakini ikapata pigo la majeraha kwa washambuliaji wake wawili, Roic Remy na
Diego Costa, ambao hawataweza kucheza mechi dhidi ya Manchester United mwishoni
mwa juma. Barcelona ya Uhispania pia iliibwaga Ajax ya Uholanzi kwa
magoli 3-1, nyota wake Neymar na Lionel Messi wakitikisa nyavu.
No comments:
Post a Comment