Wednesday, 22 October 2014

HAI KINARA WA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATOTO.


Imeelezwa kuwa wilaya ya Hai imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto mbalimbali  zinazowahusu watoto baada ya kufanya utafiti  mwaka 2010 na kuja na mkakati wa kuyashuhulikia matatizo hayo.

Akizungumza na waandaaji wa vipindi vya watoto kutoka kampuni ya TRUE VISSION, kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Bw. Zabdiel Moshi amesema  kuwa watoto wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukatili  na kutelekezwa ambao unahitaji kufanyiwa utafiti na viongozi wa eneo husika.

Akitolea mfano wilaya ya Hai amesema utafiti huo uliwawezesha kubaini sababu mbalimbali zinazosababisha watoto kunyanyasika na kukosa matunzo ya wazazi  na kusababisha  watoto kusafirishwa  sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwafanyisha kazi

Amezitaja  sababu hizo kuwa Mji wa Hai kuwa karibu na eneo la machimbo ya madini  ya Mirerani  ambayo imesababisha baadhi ya wanaume wamekuwa na mahusiano na hivyo kupata watoto ambao baade wamekuwa wakitelekezwa,sababu nyingine ni  kuporomoka kwa zao la kahawa kumechangia familai nyingi kushindwa kutoa mahitji ya msingi kwa watoto hasa kuwaendeleza kielimu kwakuwa hapo mwanzoni wazazi wengi walikuwa wanatumia zao la kahawa kama kitegauchumi.

Hata hivyo amesema uhamasishaji umefanyika kupitia  redio Boma na kamati za ulinzi wa mtoto zilizopo  ndani ya Halmsahuri uliowezesha kutoa elimu kwa jamii,mkakati mwingine ni kuanzishwa kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na kuhusisha vijana na wakina baba kujiunga na vikundi hivyo huku akitaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kupunguza vituo vya watoto kutoka 22 hadi 7 huku watoto 243 wakiwa tayari wameunganiishwa na familia zao sambamba na mafanikio mengine ambayo ni kuwepo kwa kituo shirikishi .

Katika hatua nyingine ametoa fursa kwa halmashauri nyingine kuja kujifunza katika halmashauri ya wilaya ya Hai juu ya kuimarisha ulinzi wa mtoto.

NA RIZIK LESUYA

No comments:

Post a Comment