WATUMISHI wa wawili wa
kitendo cha ardhi Wilayani Longido pamoja na Askari polisi mmoja wa kituo cha
polisi cha Wilaya Siha, wamejeruhiwa na wananchi wa kijiji cha Elerai Wilaya
Longido wakati wakifanya tathimini ya mipaka kati ya wilaya hizo mbili
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka kwa mkuu wa polisi wa wilaya Siha, Litsuya Mwakyusa alisema kuwa tukio
hilo limetokea Oktoba 22 majira ya mchana wakati watumishi hao wakiwa katika
zoezi hilo la tathmini ya upimaji wa mipaka
wa wilaya hizo mbili.
Mwakyusa alisema kuwa
katika tukio hilo
wananchi wa kijiji hicho ambayo ni jamii ya wafugaji wa kimasai waliokuwa
katika kundi waliwavamia maafisa hao na askari walikuwa wakiangalia hali ya
amani na kuwajeruhi kisha kuwapora bunduki moja
na kutoweka nayo.
Alifafanua kundi la wananchi ambalo lilikuwa likiongozwa
na vijana wa kimasai waliwajeruhi
maafisa hao kwa kutumia silaha za jadi na kuwasababishia majeruhi sehemu
mbalimbali za mwili .
Akielezea mazingira ya
tukio hilo
Mwakyusa alisema kuwa, watumishi walikuwa wakinyoosha mipaka ya wilaya hizo
mbili ili kuondoa mgogoro wa mipaka kati
ya wilaya hizo mbili uliodumu kwa mda mrefu
Hata hivyo alifafanua
kuwa, majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Kibongoto wilaya Siha na Jeshi la polisi mkoani Arusha linaendelea na
msako kwa ajili ya kuwabaini waliochukua silaha hiyo na hakuna mtu yeyote
alikamatwa kuhusiana na tukio hilo .
No comments:
Post a Comment