Wananchi wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro
wameshauriwa kujenga mtandao wa kuwapenda watu wenye ulemavu na kuwaona wenye
uwezo kama watu wengine nainapo takikana
msaada wapatiwe.
Hayo yamebainisha na mchungaji EMANUELI SWAI katika warsha ya kina mama mwenye watoto walemavu na wanao walea watoto wilayani Hai ambapo warsha hiyo imeandaliwa na shirika la Thekesho Trust Club la kuwahudumia watoto walemavu na kutoa mafunzo kwa wenye kuwalea watoto hao.
Mchungaji Swai amesema kuwa mlemavu si mtu kapenda ni mapenzi ya mungu haipasi mtu akiwa mlemavu atengwe alisema kuna sababu nyingi zinazoweza kutokea na mtu akajikuta amekuwa mlemavu alisema wapewe masomo
Amesema changamoto walizokabiliana nazo nivikwazo vyenye mtazamo wajami ubaguzi katika familia unyanyapaa. Mashuleni Hospitalini wengine wanaitwa taira.
Ametoa ushauri eneo la Ofisini zitengwe maeneo yanayoweza mtu mwenye ulemavu wamiguu aweze kupita na kibaiskeli chake bila matatizo pia wenye upungufu wa macho wawe na vifimbo vya kumsaidia na vitabu vilivo na mwinuko.
Hata hivyo mratibu wa mafunzo hayo Bibi DOROTHY NJAU pamoja na Kikosi Kazi cha wilaya ya Hai amesema Semina hiyo imepangwa vituo vifuatavyo:- Masama Mula,Masama Mashariki, Narumu Kaskazini, Machame Magharibi na Rundugai
No comments:
Post a Comment