Rais wa
Nigeria Goodluck Jonathan amesema mafanikio ya nchi yake dhidi ya maradhi ya
Ebola yametokana na imani ya wananchi wa kawaida kwa maagizo yaliyotolewa na
serikali, kuwataka wabadili mienendo yao ya kila siku maishani kama vile
kusalimiana kwa kupeana mikono, na utaratibu wa mazishi.
Amesema serikali yake ilikuwa na wasiwasi kwamba makanisa
yangekataa kuitikia wito huo katika suala la komunio ambapo watu wapatao 1000
waweza kushiriki kikombe kimoja.
Ameyasifu makanisa kwa kuusimamisha utaratibu
huo, na hata ule wa kutakiana amani wakati huu wa kitisho cha Ebola.
Kauli ya Rais Jonathan inafuatia tangazo la Shirika la afya
ulimwenguni WHO hapo jana, kwamba Nigeria sasa ni nchi isiyokuwa na
maambukizi ya Ebola, baada ya kutimiza siku 42 bila maambukizi yoyote mapya.
Siku chache kabla, Senegal
pia ilikuwa imetangazwa kuushinda ugonjwa wa Ebola.
WHO imesema hatua hiyo ni
ya matumaini kwamba maradhi hayo hatari yanaweza kuzuiliwa.
No comments:
Post a Comment