Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amelala
gerezani usiku wa kuamkia leo, akianza kutumikia kifungo cha miaka mitano
alichohukumiwa jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuuwa bila kukusudia
mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari mwaka jana.
Waendeshamashtaka walikuwa wamependekeza kifungo cha miaka 10,
lakini mawakili wake walitaka apewe kifungo cha nyumbani na kufanya kazi zenye
manufaa kwa umma. Hivi ndivyo jaji aliyeendesha kesi hiyo Thokozile Masipe
alivyosema kuhusu hukumu aliyoiona inamfaa Pistorius kwa uhalifu alioutenda.
Akizungumza nje ya mahakama baada ya hukumu hiyo kutolewa, baba
mdogo wa Oscar Pistorius alisema familia yao
imeikubali adhabu iliyotolewa na mahakama, na kuahidi kuwa mtoto wao ataitumia fursa
hiyo kutoa malipo yake kwa jamii.
Marehemu Reeva alikuwa na shahada ya sheria na mwanamitindo
maarufu nchini Afrika Kusini. Alipigwa risasi na Pistorius ambaye amesema
alimdhania kuwa mwizi aliyekuwa akijificha katika choo chake.
Na Dw Swahili
No comments:
Post a Comment