Tuesday, 21 October 2014

WIZI WA UMEME KILIMANJARO WASABABISHA VIFO.


Moshi.

WATU saba wamefariki dunia , mkaoani Kilimanjaro,akiwemo mzee mmoja Mwenye umri wa Miaka 83, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, kutokana na wizi wa kujiunganishia umeme, kinyume cha sheria.

Mzee huyo ambaye ni mkazi wa eneo la kijiji cha Otaruni kata ya kibosho kati,  alifariki baada ya kujiunganishia umeme kutoka kwenye nyumba ya mtoto wake,baada ya nyumba yake kukatiwa umeme kutokana na kulimbikiza madeni.

Mhandisi mthibiti wa mapato wa shirika la Tanesco mkoa wa Kilimanjaro,  Bakabuje Joseph, alisema kumekuwepo na wizi mkubwa  wa miundombinu ya umeme  kwa baadhi ya wananchi kujiunganishia  umeme hali iliyoisababishi shirika hilo hasara ya zaidi ya milioni 110.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mhandisi huyo alisema wananchi wengi wamekuwa na tabia ya kujiunganishia  umeme kinyume na taratibu za Tanesco jambo ambalo limepekea kupoteza rasilimali watu.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa shirika hilo mkoani Kilimanjaro Mathias Msolongo, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuharibu miundombinu hiyo, na kuwataka wananchi kufuata sheria.

Alisema  alisema  vifo vingi vya watu vimeendelea kuongezeka kutokana na wananchi kutoheshimu sheria, kutokana na tatizo hilo shirika hilo linaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya kuiba umeme.

NA mwandishi wetu.

No comments:

Post a Comment