Umoja wa Mataifa umesema kuwa kampeni ya mauaji inayofanywa na
kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS dhidi ya jamii ya wayazidi ambao ni
wachache nchini Irak, yaweza kuchukuliwa kama
jaribio la mauaji ya halaiki.
Hayo yametangazwa na naibu katibu mkuu wa umoja huo anayehusika
na haki za binadamu Ivan Simonovic, baada ya kurejea kutoka ziarani nchini
Irak.
Somonovic amesema IS imekuwa ikiwashurutisha wayazidi kubadilisha dini na
kuwa waislamu, na kutishia kuangamiza wote watakaokaidi matakwa hayo ili
kumaliza kabisa dini yao .
Mwezi Agosti mwaka huu rais wa Marekani Barack Obama
aliidhinisha mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la IS, kwa madhumuni ya kuzuia
mauaji ya halaiki dhid ya wayazidi ambayo kundi hilo lilikuwa likiazimia kuyafanya baada ya
kuyateka maeneo makubwa kaskazini mwa Irak.
No comments:
Post a Comment