Moshi.
SERIKALI imeombwa kuziondolea kodi
shule za sekondari zinazomilikiwa na Jumiya ya wazazi (CCM), mkoani Kilimanjaro
kutokana na shule hizo kutokujiendesha kibiashara.
Hayo yamesemwa na katibu wa Jumuiya
ya wazazi mkoani hapa, Selemani Pinde wakati akizungumza na waandishi wa habari
jana ofini kwake, na kuiomba serikali kuzipatia ruzuku kwa kuwa shule hizo hazijiendeshi kibiashara.
Alisema Jumuiya hiyo imekuwa
ikitoa huduma ya kielimu kwa watoto ambao wazazi wao ni wakulima na wafugaji
ambao hali zao ni duni, kwa hali hiyo wengi wao hawawezi kumudu kulipa
ada kubwa kama vile shule zingine ambazo
zimekuwa zikijiendesha kibiashara.
Katibu huyo alitolea mfano wa
Jumuiya hiyo ilitozwa kodi na TRA, baada ya wafadhili kutoka nchi ujerumani
walitoa ufadhili wa kompyuta kwa ajili ya kuisaidi shule ya sekondari ya Mwanga,
na kwamba Mamlaka hiyo, waliwatoza kiasi cha shilingi milioni 10.
Aidha Pinde alifafanua kuwa Jumuiya
hiyo hadi sasa inasomesha wanafunzi 48 ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Jumuiya hiyo ambayo inamiliki shule
tisa katika mkoa wa Kilimanjaro, pia inamkakati wa kuanzisha chuo cha ualimu
katika majengo yaliyokuwa ya shule ya sekondari ya Namfua.
NA Omary Mlekwa 0757- 357952
No comments:
Post a Comment