Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Thursday, 23 October 2014

FANYIENI KAZI CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA


WANANCHI wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufanya uchambuzi wa changamoto za mazingira zilizopo ili waweze kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha mazingira ya wilaya hiyo yanatunzwa na kuwa katika hali nzuri muda wote.

Hayo yalisemwa na Maggece Simbaye ambaye ni Meneja wa the Dare Women's Foundation[DWF]kutoka mkoani Arusha wakati alipotombelea Taasisi ya TAKIMA inayojishughulisha na utetezi wa haki za jamii iliyopo katika Kijiji cha Nkusinde kata ya machame mashariki wilayani Hai amabapo pia walitundika mizinga 10 katika mto weru weru na kutembelea watoto yatima wa maeneo hayo.

Simbaye alisema suala la utunzaji mazingira siyo la mtu mmoja au kikundi flani,bali ni jukumu la watu wote ambalo linahitaji ushirikiano na uwajibikaji wa pamoja na wadau wote wanaohusika na uhifadhi wa mazingira.

Alisema ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,wananchi wanatakiwa kuepuka  ukataji miti hovyo,uchomaji moto wa misitu na uoto wa asili, kupanda miti na kuitunzapamoja na  kuthibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za viwandani na makazi

Kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya Takima andrea Njau amesema licha ya taasisi yake kujishughulisha na shughuli ya kutetea jamii pia wanajishughulisha na utunzaji  wa mazingira na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira

Sambamba na hilo wameanza mradi wa ufugaji wa nyuki katika kijijiji cha nkusinde katika mto weru weru na wameanza na mizinga kumi na matarajio ilikufikisha mizinga 300 ili kujiongezea ajira kwani ufugaji nyuki nimradi raisi  usio hitaji gharama kubwa na soko la asali linapatikana hivyo kuwataka wananchi kujiunga na mradi huo

NA MWANDISHI  WETU

ASKARI POLISI NA WATUMISHI WAJERUHIWA NA WAFUGAJI WILAYANI LONGIDO


WATUMISHI wa wawili wa kitendo cha ardhi Wilayani Longido pamoja na Askari polisi mmoja wa kituo cha polisi cha Wilaya Siha, wamejeruhiwa na wananchi wa kijiji cha Elerai Wilaya Longido wakati wakifanya tathimini ya mipaka kati ya wilaya hizo mbili

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mkuu wa polisi wa wilaya Siha, Litsuya Mwakyusa alisema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 22 majira ya mchana wakati watumishi hao wakiwa katika zoezi hilo la tathmini ya  upimaji  wa mipaka  wa wilaya hizo mbili.

Mwakyusa alisema kuwa katika tukio hilo wananchi wa kijiji hicho ambayo ni jamii ya wafugaji wa kimasai waliokuwa katika kundi waliwavamia maafisa hao na askari walikuwa wakiangalia hali ya amani na kuwajeruhi kisha kuwapora bunduki moja  na kutoweka nayo.

Alifafanua  kundi la wananchi ambalo lilikuwa likiongozwa na vijana wa kimasai waliwajeruhi  maafisa hao kwa kutumia silaha za jadi na kuwasababishia majeruhi sehemu mbalimbali za mwili  .

Akielezea mazingira ya tukio hilo Mwakyusa alisema kuwa, watumishi walikuwa wakinyoosha mipaka ya wilaya hizo mbili ili kuondoa  mgogoro wa mipaka kati ya wilaya hizo mbili uliodumu kwa mda mrefu

Hata hivyo alifafanua kuwa, majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Kibongoto wilaya Siha na  Jeshi la polisi mkoani Arusha linaendelea na msako kwa ajili ya kuwabaini waliochukua silaha hiyo na hakuna mtu yeyote alikamatwa kuhusiana na tukio hilo.

NA Omary Mlekwa 0757357952