Friday, 6 March 2015

DC ISOMENI KATIBA PENDEKEZWA KWANZA



Wananchi wilayani hai mkoani Kilimanajaro wametakiwa kuisoma na kuielewa katiba pendekezwa na hatimaye kuipigia kura ili kupata katiba mpya yenye kukidhi matakwa ya wananchi.

Hayo yamesemwa hii leo na mkuu wa wilaya mshikizi Novatus Makunga ambaye pia ni muu wa wilaya ya Moshi wakati wa uzinduzi wa katiba pendekezwa  uzinduzi ambao umehudhuriwa na viongozi wa serikali na taasisi mbali mbali zisizo za kiserikali.

Makunga amesema kuwa ni vyema wananchi wakatumia muda wao kuzisoma nakala za katiba pendekezwa zitakazotolewa katika maeneo yao na kuepukana na watu wanaoizungumzia katiba hiyo  pendekezwa bila ya kuwa na uelewa wa kile kilichoandikwa.

Awali akimkaribisha mkuu wa wilaya mshikizi, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Melkizedeck Humbe amesema kuwa nakala hizo zitagawiwa katika kata, vijiji, zahanati, hospitali, vyuo na taasisi mbali mbali bila kusahau vijiwe mbali mbali vilivyopo wilayani hapa huku pia akimtaka kila mwananchi kuisoma katiba hiyo pendekezwa.

Naye mwenyekiti wa baraza la madiwani wa Hai Clement Kwayu amesema kuwa mwananchi ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ambapo maamuzi hayo yatatolewa katika kura ya maoni ambapo kila mwananchi atapata fursa ya kushiriki kuipigia kura.

Kwa upande wake afisa habari wa wilaya ya Hai bi. Rizik Lesuya amesema kuwa wananchi watapata kuielewa katiba pendekezwa hasa ukizingatia halmashauri ya Hai inamiliki kituo cha redio Boma hai Fm ambacho kitafanya kazi ya kuuelimisha umma juu ya katiba pendekezwa kupitia vipindi vyake.

NA
Edwine Lamtey 0758-129821


MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUFANYIKAHAPOKESHO

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro yanatarajiwa kufanyika hapo kesho katika ukumbi wa Halmashauriya wilaya Hiyo.
mkuu wa idaraya maendeleo ya jamii anawakaribisha wananchi wote kuhudhuria katika kilele cha maadhimisho hayo.

Thursday, 22 January 2015


mkurugenzi mtendaji (w) Hai Melkizedeck Humbe akikagua kisima kidogo kabla ya kuwasili kwa kamati ya bunge ya maji.
picha na Edwine Lamtey




watatu katika picha ni mhandisi wa maji wilaya pamoja na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Hai wakiangalia Water division chanber ya mradi wa Lyamungo Umbwe. 











katika picha ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai ndugu Melkizedeck Humbe  akiongozana na kamati ya maji ya Bunge ambayo ilifika wilayani Hai kwa aajili ya kukagua na kutathimini miradi ya maji eneo walilopo ni eneo la Machame Narumu katika Subdivision ya mradi wa Lyamungo Umbwe

picha na Edwine Lamtey 0758-129821



mbunge wa jimbo la Babati bwana Jonson Jitu akisalimiana na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ndugu Clement Kwayu  wapili kushoto kwa mwenyekiti wa halmashauri ni mhandisi wa maji wilaya Eng. Nyakaraita Mwita.
picha na Edwine Lamtey 0758-129821

Wednesday, 21 January 2015



nini chanzo cha kukatika kwa umeme wakati tunamitambo mizuri? ni baadhi ya wananchi wa maeneo ya songea wamehoji huku pia mkoani Kilimanjaro wilayani Hai wananchi wametoa kero hiyo katika kipindi cha Siku mpya wakitaka kujua nini chanzo cha kukatika kwa umeme huku pia wakiomba wahusika kutoa taarifa ya katizo la umeme kama kuna tatizo.

WAWILI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA


Afisa biashara wa  Halmashauri ya wilaya ya Hai bwana Halfan Kimaro akizungumza na wananchi waliohudhuria katika ufunguzi wa ofisi za mobisol wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kulia kwake ni Mwendesha tawi la mobisoli Tawi la Bomang’ombe Abubakari Mohamed



hizi ni baadhi ya bidhaa za Mobisol ikiwemo solar tv ya mobisol na vifaa vingene kwaajili ya nishati hiyo 
picha na Edwine Lamtey


MOBISOL   YAANGAZA WILAYA YA HAI


WANANCHI wilayania Hai Mkoani Kilimanjaro wameshauriwa kuepuka usumbufu wa upatikanaji wa nishati uliopo kwa kutumia sola ili kurahisisha gharama na kuepuka usumbufu.

Rai hiyo imetolewa leo na Afisa Biashara wa wilaya ya Hai Kimaro alipokuwa akizindua ofisi ya kampuni ya sola ya Mobisol ili kurahisisha na kuwapatia wananchi wa mjini na vijijini huduma ya umeme wa sola.

Kimaro amesema kuwa tatizo la Umeme limekuwa likiwakosesha wananchi kufanya mambo yao muhimu hasa yakimaendeleo yanayo hitaji nishati huku hali ya idadi ya Wakazi wilayani Hai ikiongezeka siku hadi siku.

Amesema kuwa ni vema kila Mwananchi kulinda kipato chake na kuondokana na tatizo la umeme katika maeneo yao kwa kuwa na huduma ya sola hiyo huku wakiambatanisha na nishati nyingine kama tahadhari na kwa matumizi mengine.

Awali  Mwendesha tawi la mobisoli Tawi la Bomang’ombe Abubakari Mohamed amewataka wananchi wa Hai na viunga vyake kutumia pesa kwa malengo huku wakipata huduma ya nishati ya Sola kwa bei nafuu ili kulinda kipato cha Familia 

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kukumbuka pia wazazi wao walio vijijini kwa kuwapatia nishati ya Umeme wa Sola ili waweze kufanya mambo yao wawapo vijijini kwani upatikanaji wa umeme baadhi ya  vijijini umekuwa ni shida.

Habari na Davis Minja 0769432367







WATU wa wili wakazi wa wilaya ya Hai Kijiji cha Uduru Machame Mkoani Kilimanjaro wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai Denis Mpelembwa,Mwendesha Mashtaka wa Polisi Inspekta Simon Feo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hendry Loti Masawe mwenye umri wa miaka 30 na mwenzake Abiudi Jubilet Shilewangwa mwenye umri wa miaka 35 wote wakazi wa Machame.

Aidha  watuhumiwa hao wamekutwa na hatia hiyo baada ya ushahidi uliokuwa  kukamilika ambapo watuhumiwa hao walitenda kosa hilo huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria ambapo pia mshitakiwa wa kwanza Hendry Loti  Massawe ni  shemeji wa Mwanafunzi huyo.

Kesi hiyo kwa mara ya kwanza iliripotiwa katika Dawati la Jinsia La Wilaya Ya Hai chini ya Mwenyekiti wa dawati hilo Happyness Eliufoo ambapo ilifikishwa mahakamani kwa upelelezi zaidi hadi upelelezi ulipo kamilika na kutolewa kwa hukumu.

Awali watuhumiwa hao walimbaka Mwanafunzi huyo kwa zamu Disemba 26 mwaka 2013 huko katika kijiji cha Uduru Machame Wilayani Hai ambapo shemeji yake Hendry Loti Massawe alimshawishi kutoka naye wakasherehekee sikukuu ambapo ilikuwa kinyume kisha kumbaka  nakumsababishia maumivu makali.

Mwenyekiti wa dawati la polisi wilaya ya Hai Happyness Eliufoo amesema kuwa ni vyema taarifa zaidi zikaendelea kutolewa kwa wale wanaofanya ukatili na unyama dhidi ya binadamu na kusema kuwa huku hii pia ni fundisho kwa wale wenye tabia kama hizi.

Habari na Devis Minja  0769-432367



Tuesday, 20 January 2015

Hospitali ya Bugando yapunguza gharama za upasuaji wa moyo


Hospitali ya Bugando imepunguza gharama za upasuaji wa moyo kutoka kati ya shilingi milioni tatu hadi kufikia shilingi elfu hamsini tu.
Hospitali ya rufaa Bugando iliyopo jijini mwanza imepunguza gharama za upasuaji wa moyo, kutoka kati ya shilingi milioni tatu hadi nane ilizokuwa inawatoza wagonjwa kwa upasuaji mkubwa na mdogo hadi kufikia shilingi elfu hamsini tu ili kuwawezesha wananchi wengi wasio na uwezo wa kumudu gharama hizo kunufaika na matibabu hayo.

Mkuu wa idara ya upasuaji wa moyo na kifua katika hospitali ya rufaa Bugando Prof. William Mahalu amessema kutokana na ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa moyo, zaidi ya watoto 20 wanaopata huduma ya kliniki katika hospitali hiyo pamoja na watu wazima 25 wamekuwa kila mwezi wakigundulika kusumbuliwa na tatizo la moyo, ambapo mwaka huu watoto 10 wamegundulika na tatizo hilo na watoto sita wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka.
 
Daktari bingwa wa kitengo cha upasuaji wa moyo kwa watoto katika hospitali hiyo Dk. Godwin Sharau pamoja na kuzishukuru taasisi za nje ya nchi, wadau na marafiki wa hospitali ya rufaa Bugando waliosaidia operesheni za moyo kufanikiwa kwa gharama nafuu kabisa, amesema mwaka huu lengo ni kuwafanyia operesheni wagonjwa 100 na miaka mitatu ijayo ni kufikia wagonjwa 250 kwa mwaka.
 
Mkuu wa wilaya ya Kwimba Selemani Mzee amesema huduma hiyo inayofanywa na idara ya upasuaji wa moyo na kifua inapaswa kuwafikia wananchi wengi hususani wa vijijini ambao pamoja na kusumbuliwa na tatizo hilo lakini wanahofia gharama kubwa ya matibabu, huku mzazi wa mtoto Lukaiya Shaban Bw. Shaban Juma Ramadhan ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa moyo na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo katika hospitali hiyo akishukuru kwa huduma hiyo.
 
Upasuaji wa moyo katika hospitali ya rufaa Bugando ulianza miaka saba iliyopita, ambapo hadi kufikia mwaka jana 2014, hospitali hiyo ilikuwa na jumla ya wagonjwa 769 waliokuwa wakingoja kufanyiwa upasuaji, aidha katika kipindi hicho watoto 44 walipelekwa Israel, 38 walitibiwa katika hospitali hiyo – ambapo 14 walifanyiwa upasuaji na madakatari bingwa wa moyo kutoka Australia na wengine 24 walifanyiwa upasuaji na timu ya madakatari wa hospitali ya Bugando.