Wednesday 19 November 2014

CRDB Bank tunasiliza wateja














kushoto katika picha ni mkurugenzi wa CRDB kanda ya kaskazini ndugu Fransis Moleli na wapili ni meneja wa crdb-Hai ndugu Shirima huku  watatu ni meneja wa CRDB-siha bi. Lightness Tarimo wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo kibong'oto wilayani siha wakati walipokabidhi magoro, vyandarua na sabuni hospitalini hapo.

Picha na Edwine Lamtey

















katika picha aliyeshikilia godoro ni mmoja kati ya wauguzi hospitali ya kibong'oto akipokea msaada wa magoro yaliyotolewa na banki ya CRDB-Siha

Picha na Edwine Lamtey 0758-129-821



Tuesday 18 November 2014

CRDB- SIHA YAMWAGA MAGODORO,VYANDARUA NA SABUNI HOSPITALI YA KIBONG'OTO.




Benki ya CRDB inayomjali na kumsikiliza mteja kupitia tawi la Siha lililopo  mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Siha imewatembelea wateja wake katika hospitali ya Kibong’oto ambapo wamegawa magodoro,mashuka na sabuni kwa ajili ya watoto na kuahidi kuwa bado itaendelea kutoa misaada mbalimbali ili kujenga mahusiano makubwa zaidi na wateja wao.


Akikabidhi msaada huo mkurugenzi wa benki ya CRDB mkoa Kilimanjaro Fransis Moleli amesema kuwa banki hiyo inatambua umuhimu wa wateja wake hivyo kwa kupitia siku ya wateja duniani(CUSTOMER SERVICE WEEK) imeamua kutoa msaada huo ili kusema Asante kwa wateja wake.



Akipokea msaada huo daktari mkuu katika hospitali ya kibong’oto Dr. Kisonga Riziki amesema kuwa anaishukuru benki ya CRDB kwa msaada walioutoa hii ikiwa ni njia pekee ya kuendelea kuwajali wateja wake pamoja na kushiriki huduma za kijamii na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake meneja wa CRDB-Siha bi. Lightness Tarimo amesema kuwa katika kupanua huduma za kifedha CRDB ina mfumo wa kufanya miamala mbali mbali kwa njia ya simu iitwayo SIMBANKING hivyo ni vyema wananchi wakatumia fursa hiyo ili kujipatia huduma kwa urahisi. 

Pia amewakaribisha wafanyakazi wa hospitali hiyo  kujipatia  huduma mbalimbali kama vile mikopo,kufungua akaunti n.k
Aidha pia Bi. Lightness amesema kuwa msaada ambao umetolewa ni ishara ya kuonyesha kuwa  benki itazidi kushirikiana na hospitali hiyo pamoja na vyombo vingine vinavyotoa huduma kwa jamii ili kuimarisha mahusiano mazuri zaidi kwenye utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Hospitali ya kibong’oto ni hospitali maalumu ya kutoa huduma kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kifua kikuu na magonjwa mengine.
Na Edwine Lamtey

Thursday 6 November 2014

WAALIMU WAPEWE HAKI ZAO ZA MSINGI.




WITO umetolewa kwa serikali kuepusha migogoro ya kimaslahi baina ya waalimu na serikali  kuwapa waalimu haki yao ya msingi ya kupata mshahara kwa wakati.

Hayo yamesemwa  na katibu wa chama cha waalimu wilaya ya hai Samweli Nyakrere wakati akizungumza na redio Boma Hai Fm ofisini kwake.

Amesema kuwa kutokana na madai ya muda mrefu kutokea mwaka 2008 kutokupewa kipaumbele katika kulipwa kwa wakati hali inayochangia kuwepo kwa migogoro baina ya serikali na waalimu.

Ameongeza kuwa katika upandishwaji wa madaraja  kwa waalimu bado hawapandishwi madaraja jambo linalo pelekea waalimu kukata tamaa na kazi yao huku sera ya serikali ikiwa ni matokeo makubwa sasa.

Kwa upande wake meneja wa saccos ya waalimu wilaya ya hai bi. Pendo Lyatuma  amesema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa serikali wameweza kutoa mikopo kwa riba nafuu kwa wafanyakazi wa serikali na wasio wa serikalini pamoja na kuwapa mikopo waalimu kusoma na kuongeza elimu yao.

Aidha Lyatuma ametoa wito kwa wanachama kuona umuhimu wa kuweka akiba katika saccos wanazo kopa kwaajili ya kuwasaidia kwa maisha ya baadae.

Na Latifa Boto.

MBOWE - HAI LAZIMA IWE SAFI KUANZIA SASA







Mbunge Wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro  Freeman Mbowe amesikitishwa na kitendo cha mji mdogo wa hai kuendelea kuwa na uchafu, pamoja na kwamba aliaznisha mpango wa kusafisha mji huo.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara ulio fanyika  katika  mji mdogo wa bomang'ombe amesema kuwa kitendo cha madiwani kushindwa kutekeleza  mpango wa kufanya usafi kimemsikitisha jambo ambalo limemlazimu kutafuta mbinu mbadala.

Mbowe amesema pamoja na viongozi hao kushindwa  kusimamia suala hilo la usafi ameamua kuweka mikakati thabiti itakayo saidia kuondokana na hali ya mji kuwa mchafu kwa kutoa vitendea kazi mbalimbali kwaajili ya kufanyai usafi.

Amefafanua kuwa  ili kukabiliana na hali ya uchafu ametoa gari la kubeba taka lenye tani 30 kwaajili ya kubeba taka katika masoko mbalimbali ndani ya wilaya ili kunusuru afya za walaji na wafanya biashara wanaotoa huduma mbalimbali katika masoko yaliyo ndani ya wilaya ya hai kama vile soko la walaji Hai mjini, soko la masama mula, soko la kalali pamoja na masoko mengine.

Akizungumzia suala zima la huduma ya afya amesema kuwa ili kuondokana na tatitio la gari maalumu la kubebea wagonjwa (ambulance) ameahidi kutoa gari la wagonjwa kwa hosipitali teule ya Machame na katika hosipitali ya wilaya ya Hai.

Mh. Mbowe ameongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa njia zina fanyiwa ukarabati wa kiwango kinacho ridhisha na kufungua njia nyingine kwaajili ya manufaa ya wananchi  ametoa  greda itakayo baki ndani ya wilaya siku zote kwa kuchimba na kuchonga barabara ndani ya wilaya nzima ya Hai ili kurahisisha usafiri. 

Aidha pia Mbowe amewataka wananchi kuchagua viongozi waadilifu na watenda haki katika uchaguzi  wa mwezi ujao  desemba wa  uchaguzi wa viongozi wa serikali ya mitaa ili waeweze kutetea haki ya mtanzania.


Na Devis Minja.
picha na Edwine Lamtey.

Wednesday 5 November 2014






mbunge wa jimbo la Hai Mh. Freeman Mbowe akizungumza na wananchi wa jimbo la Hai katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya snow view  vilivyopo katika mji wa bomang'ombe.  

picha na Edwine Lamtey


pichani ni wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo pamoja na wananchi wa wilaya ya Hai waliokusanyika huku wakimshangilia mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema  Taifa Mh. Freeman Aikael Mbowe wengi wa wafuasi hao wilayani hai hupenda kumuita ''Kaka''. 

Picha na Edwine Lamtey

Thursday 23 October 2014

EBOLA YAZUA HOFU KWA WANANCHI MOSHI


Wananchi mkoani Kilimanjaro wamekuwa na taharuki ya ugonjwa wa ebola mkoani hapo baada aliyedaiwa kuwa mgonjwa wa ebola kufikishwa katika kituo cha shirimatunda ambacho kimetengwa na mkoa kwa ajili ya kushughulikia suala hilo.

Na kwa taarifa zilizopo hadi sasa ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amethibitisha kuwa “ni kweli kituo  cha shirimatunda kimetengwa kwaajili ya watu wenye ugonjwa wa ebola kufanyiwa uchunguzi, ila kwa mgonjwa aliyefikishwa hapo amepimwa na kuonekana hana maambukizi ya ugonjwa huo ila alihisiwa na madaktari”

 “alisema Gama”

Hata hivyo mkuu huyo wa mkuu wa mkoa atakutana na waandishi wa habari hii leo majira ya saa nne na imani ni kwamba atazungumzia suala hili.

Endelea kusikiliza redio Boma Hai Fm na kutufuatilia katika mtandao wetu kwa taarifa zaidi.

Na Edwine Lamtey 0758-129 821