Sunday 18 January 2015

Kiasi ya watu 10 wauawa Niger


Kiasi ya watu kumi wameuawa katika ghasia zilizozuka nchini Niger kufuatia maandamano ya Waislamu walioghadhabishwa na kuchapishwa kwa kikaragosi cha mtume Muhammad katika jarida maalum la Charlie Hebdo.
 Rais wa Niger Mahamadou Issoufou amesema watu watano wameripotiwa kuuawa baada ya maandamano yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Niamey hapo jana na wengine watano waliuawa siku ya Ijumaa katika mji wa Zinder baada ya maandamano yaliyofanywa baada ya sala za Ijumaa.
 Waathiriwa walikuwa ndani ya makanisa na vilabu vya pombe ambayo yalichomwa na waandamanaji. Mamilioni ya Waislamu kote duniani wameghadhabishwa na kuchapishwa tena kwa kikaragosi cha mtume Muhammad na viongozi wa Kiislamu wamelaani kuchapishwa huko ambako wamekuita uchokozi na kuudunisha Uislamu.
 Kulingana na kura ya maoni iliyofanywa nchini Ufaransa, asilimia hamsini ya Wafaransa wanapinga kuchapishwa kwa kikaragosi hicho.
Maafisa wa kijeshi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq wamesema takriban watu 200 wa kutoka jamii ya walio wachache ya Yazidi wameachiwa huru na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la kiislamu IS.]
 Kamanda wa kikosi cha Wakurdi cha Peshmerga tawi la kaskazini mwa mji wa Kirkuk Shirko Fatih amesema leo kuwa karibu ya mateka hao wote walioachiwa huru ni wanaume na wanawake wazee walio katika hali mbaya ya kiafya na watoto watatu. 
Wanamgambo wa IS waliwasafirisha kutoka mji wa Tal Afar ambako wamekuwa wakiwazuia kwa miezi mitano iliyopita na kuwaacha katika daraja la Khazer karibu na mji mkuu wa jimbo la Iribil.Maafisa wa Kikurdi wamewachukua kwa ajili ya uchunguzi.

No comments:

Post a Comment