Monday 19 January 2015

MAJAMBAZI WATEKA MAGARI, WAWAVUA WANAWAKE NGUO NA KUPORA MALI


Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wameteka mabasi saba ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya na kupora mali na fedha ambavyo thamani yake haijafahamika.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la polisi, mkoani Arusha llitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mbuga Nyeupe, wilayani Longido Mkoa wa Arusha baada ya watu hao kuweka mawe barabarani na kuwamuru abiria wote kutemka mmoja baada ya mwingine, kulala chini na kuwapekua kila kitu walichokuwa nacho.
DEREVA ALIYETEKWA ASIMULIA
Akisimulia mkasa huo, dereva wa basi la Perfect Trans, Joseph John, alisema kuwa watu hao waliokuwa na silaha za jadi yakiwamo mashoka, mapanga na sime, waliteka mabasi hayo majira ya saa 8 usiku.
“Hao jamaa walikuwa kama 50 hivi kwani waliteka magari yetu ambayo yalikuwa yamefuatana, wametuvua hadi viatu, saa yaani walipekua hadi wanawake waliamriwa kuvua nguo na kuporwa urembo wenye nakshi ya madini ya vito,” alisema John.
Alisema yeye alikuwa dereva wa kwanza kufika na basi katika eneo hilo na kuwa alipoona mawe yamepangwa kati kati ya barabara, aliamua kusimama na alipokuwa akijaribu kuyakwepa, alipigwa jiwe usoni hali iliyomfanya ashindwe kukimbia.
“Hata wengine walikuwa hawajafunika nyuso zao, tukio lilidumu kwa dakika zaidi ya shirini, kila walipomaliza kupekua watu wa basi moja waliwaamuru warudi ndani ya gari,” alisimulia.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jabir Athumani, alisema baadhi ya majambazi hayo yalikuwa yakiita majina ya baadhi ya watu na kuwaamuru kutoa fedha walizokuwa nazo.
“Tunaomba vyombo ulinzi na usalama vifuatilie tukio hili kwa umakini wa hali ya juu ili kuwanasa wahusika wa tukio hili,” alisema Jabir.
Aidha, alililitaka Jeshi la Polisi lirudishe magari ya doria katika barabara ya Arusha–Namanga ambayo yaliondolewa Aprili mwaka jana.
POLISI: TUTAZUNGUMZA LEO
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi leo.
“Hapa nipo katika majukumu mengine, sipo ofisini nitawapa taarifa za tukio lote Jumatatu (leo) mchana, naomba subiri nitafanya mkutano na vyombo vya habari na nitawapa maelezo ya tukio lote,” alisema Sabas.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram, wamewateka nyara watu wapatao 80 baada ya kufanya shambulizi katika eneo la kaskazini mwa Cameroon. Polisi wa Cameroon wamesema shambulizi hilo limefanyika siku moja baada ya nchi jirani ya Chad, kupeleka wanajeshi wake kuapambana na kundi hilo.
chanzo ni DW (Kiswahili)
1 hr ·  

Sunday 18 January 2015


Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kudhibiti wanachi waliobeba madumu wakitaka kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguna katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.

SERIKALI YANUNUA BOTI YA DORIA


Serikali imekamilisha mchakato wa kununua boti maalum zitakazosaidia kuimarisha doria na ulinzi wa shughuli za uvuvi kwenye maziwa mbalimbali nchini ikiwemo ziwa Tanganyika mpango ambao utaendeshwa kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo jeshi la polisi na jeshi la wananchi.
chanzo cha habari hii ni ITV

NORWAY KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA




Serikali ya Norway imeeleza azma yake ya kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuboresha huduma za afya hususani kwa wananchi wa vijijini wanaoishi pembezoni ili waweze kupata huduma zenye uwiano sawa na wanazopata wananchi wengine.-

Kiasi ya watu 10 wauawa Niger


Kiasi ya watu kumi wameuawa katika ghasia zilizozuka nchini Niger kufuatia maandamano ya Waislamu walioghadhabishwa na kuchapishwa kwa kikaragosi cha mtume Muhammad katika jarida maalum la Charlie Hebdo.
 Rais wa Niger Mahamadou Issoufou amesema watu watano wameripotiwa kuuawa baada ya maandamano yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Niamey hapo jana na wengine watano waliuawa siku ya Ijumaa katika mji wa Zinder baada ya maandamano yaliyofanywa baada ya sala za Ijumaa.
 Waathiriwa walikuwa ndani ya makanisa na vilabu vya pombe ambayo yalichomwa na waandamanaji. Mamilioni ya Waislamu kote duniani wameghadhabishwa na kuchapishwa tena kwa kikaragosi cha mtume Muhammad na viongozi wa Kiislamu wamelaani kuchapishwa huko ambako wamekuita uchokozi na kuudunisha Uislamu.
 Kulingana na kura ya maoni iliyofanywa nchini Ufaransa, asilimia hamsini ya Wafaransa wanapinga kuchapishwa kwa kikaragosi hicho.
Maafisa wa kijeshi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq wamesema takriban watu 200 wa kutoka jamii ya walio wachache ya Yazidi wameachiwa huru na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la kiislamu IS.]
 Kamanda wa kikosi cha Wakurdi cha Peshmerga tawi la kaskazini mwa mji wa Kirkuk Shirko Fatih amesema leo kuwa karibu ya mateka hao wote walioachiwa huru ni wanaume na wanawake wazee walio katika hali mbaya ya kiafya na watoto watatu. 
Wanamgambo wa IS waliwasafirisha kutoka mji wa Tal Afar ambako wamekuwa wakiwazuia kwa miezi mitano iliyopita na kuwaacha katika daraja la Khazer karibu na mji mkuu wa jimbo la Iribil.Maafisa wa Kikurdi wamewachukua kwa ajili ya uchunguzi.

Monday 22 December 2014

PESA HIZI NI ZA NANI NAULIZA?



Rais Kikwete asema: Waziri wa ardhi, tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. 
Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.